Wednesday, February 19, 2014

MIKOSI YAZIDI KUMUANDAMA SHILOLE YALIYOMKUTA IGUNGA HAYASIMULIKI JAMANI, WANCHI WAMPIGA MARUFUKU KUKANYAGA HUKO KISA?


Wananchi mbalimbali wakishangaa mapaja ya
Shilole
Maskani ya Mung wee, watoto wadogo
wakimshangaa Shilole jinsi.
Na Mwandishi wa Xdeejazy Igunga
Ile Ziara ya wanamuziki Mad, Queen Durleen
na Shilole imeingia doa kufuatia wananchi
wengi kutokufurahishwa na uvaaji aliokuwa
ameuvaa Shilole huku wazee wa Kisukuma na
Kinyamwezi kumlani vikali mwanamuziki huyo
na kudai siku akirudi tena huko aje amevaa
gauni la sivyo atakiona cha moto.
Mtonyaji wetu wa habari hizi ambae alikuwa
kwenye msafara wa wasanii hao aliieleza
Xdeejayz kuwa Shilole aliwafanya wakazi hao
kushindwa kufurahia ujio wa wanamuziki hao
kutokana na kingu kifupi alichokuwa amevaa
huku sehemu ya mapaja yake ikiwa wazi na
watoto kushuhudia nusu mwili wake jambo
ambalo hawajawahi kuona.
Hata hivyo Shilole ambae amekuwa na kawaida
ya kuvaa nusu uchi akiwa stejini jambo ambalo
mashabiki wengi wamekuwa wakichukizwa nalo
na wamekuwa wakimuonya mara kwa mara
kuachana na kuvaa nusu uchi kwa vile
mashabiki wengi wanahitaji burudani na sio
kuona maungo ya miili yake, lakini ameonekan
kupuuza.
Xdeejayz ilimtafuta Shilole kupitia simu yake
ya kiganjani ili azungumzie balaa hilo lililom
kuta lakini kwa bahati mbaya hakuweza hadi
habari hii inawafikia wasomaji wetu wenye kiu
ya kujua habari na matukio yalijiri wikiend.

1 comment:

.