Thursday, February 27, 2014

MIMBA YA LINAH YACHOROPOKA


SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa,
msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga
‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye
Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito
huo umechoropoka .
Astelinah Sanga ‘ Linah’.
Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo
umechoropoka hivi karibuni na kumfanya
Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake
ilikuwa kupata mtoto .
“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini
umetoka na amesikitika sana kwani mdosi
wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye
alitamani sana kuwa na mtoto, ” kilisema
chanzo hicho .
Gazeti hili lilimtafuta Linah kupitia simu
yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa
kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya
mwindishi wetu kujitambulisha , staa huyo
alikata simu .
Wiki iliyopita gazeti dada na hili , Risasi
Mchanganyiko la Februari 19- 21 , mwaka
huu liliandika habari za staa huyo kunasa
ujauzito wa mdosi huyo na alipoulizwa
alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.
“Nani kakwambia kwamba nina mimba ?
Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza
mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini
miye sina mimba , ” alisema Linah na
kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka
mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na
habari motomoto za masupastaa.

No comments:

Post a Comment

.