Thursday, February 27, 2014

LULU AANIKA MCHECHETO KIZIMBANI


STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘ Lulu’ amefunguka kuwa siku
alipokuwa mahakamani akisomewa kesi
inayomkabili ya kumuua bila kukusudia
msanii mwenzake , marehemu Steven
Kanumba , alipata mchecheto sana .
Elizabeth Michael 'Lulu '.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema , siku
hiyo wakati kesi ikiendelea, alipata
mchecheto kiaina na kujikuta ghafla
akiwaza juu ya hatima yake hivyo
kuangukia katika lindi la hofu .
“Daah ! Nilipata mchecheto ghafla hata sijui
kwa nini , nilivuta picha ya mbali sana na
kujikuta nikijiuliza maswali mengi
yasiyokuwa na majibu, ” alisema.
Msanii huyo alisomewa shitaka lake hilo
Februari 17 , mwaka huu kwenye Mahakama
Kuu , jijini Dar, kesi hiyo iliahirishwa hadi
itakapotajwa tena baada ya msanii huyo
kujibu maswali ya kweli au si kweli .

No comments:

Post a Comment

.