Sunday, February 23, 2014

Picha za AJALI mbaya ya malori iliyotokea Mikese Morogoro ambapo DEREVA mmoja wa lori amepoteza maisha,,,,,,,,,,,,,


Baadhi ya watu waliokwama kijiji cha Fulwe
kata ya Mikese mkoani Morogoro wakiangalia
mwili wa dereva wa lori lililobeba shehena ya
mafuta lililokuwa likitoka Dar kueleka upande
wa Morogoro, ukiwa umeteketea vibaya kwa
moto baada ya ajali.
Mwili wa dereva wa lori la mafuta ukiwa
umeteketea kwa moto.
Ajali mbaya imetokea leo katika kijiji cha
Fulwe, kata ya Mikese mkoani Morogoro ambapo
malori mawili yamegongana na kuteketea kwa
moto.
Katika ajali hiyo, dereva wa lori moja
lililokuwa na shehena ya mafuta amepoteza
maisha wakati dereva wa lori lingine aina ya
semitrela akijeruhiwa pamoja na tingo wake na
kukimbizwa hospitali.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amedai
kuwa dereva aliyepoteza maisha alishindwa
kujiokoa baada ya ajali kutokea kwa kubanwa
hali iliyopelekea kuungua vibaya kwa moto.
"Lori hili la mafuta lilikuwa likitoka Dar na
kushuka mteremeko huu kwa kasi huku
semitrela likijaribu kulipita lori lingine eneo
hili hivyo kugongana uso kwa na lori la mafuta.
Baada ya kugongana, mafuta yaliyokuwa
kwenye tenki yalimwagika hali iliyosababisha
malori yote kuteketea kwa moto. " Alisema
shuhuda huyo mkazi wa kijiji cha Fulwe, Bw
Issa Athuman.

1 comment:

  1. R.I.P DEREVA ajali uisikie tu maana mmmmh!!!! huo moto kama bomu

    ReplyDelete

.