Mama yake aiomba
jamii imsaidie
Sophia Kindamba akiwa na mwanae Junior
Richard Rutta
.....................................
MTOTO Junior Richard Rutta ambaye jinsia yake
haieleweki anatafuta msaada
utakaomuwezesha kufanyiwa uchunguzi katika
hospitali ya CCBRT, jijini Dar es Salaam.
Mtoto huyo mwenye miaka miwili na miezi saba
anaishi na mama yake mzazi, Sophia
Kindamba, mtaa wa Mtwivilla, mjini Iringa.
Akiomba msaada huo, mama yake alisema
jitihada za madaktari wa hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kuchunguza na hatimaye kujua mtoto
huyo ana jinsi gani zinaelekea kukwama.
“Kwa mara ya kwanza nilimpeleka katika
hospitali hiyo mwanzoni mwa mwaka 2012,
lakini hadi hii leo hakuna majibu yoyote;
kwahiyo haieleweki kama ni msichana au ni
mvulana” alisema huku machozi yakimtoka.
Alisema mapema mwaka huu alikwenda
Muhimbili lakini kwa majibu aliyopewa
amepoteza imani ya tatizo la mwanae
kushughulikiwa hospitalini hapo.
Kindamba alisema “nimeambiwa kipimo kile
kinatakiwa kupelekwa nje ya nchi baada ya
uchunguzi wake hospitalini hapo kushindikana.”
Alisema wakati akipewa majibu hayo
ameshauriwa akajaribu pia kupata vipimo hivyo
katika hospitali ya CCBRT.
“Nimerudi Iringa kutafuta hela ili nikienda
CCRBT nisipate shida ya gharama za uchunguzi
na matibabu,” alisema.
Kindamba alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya
Iringa leo amempa barua itakayomuwezesha
kupita kwa watu, taasisi na mashirika
mbalimbali kuomba mchango.
“Naomba mnichangie; baba wa mtoto alinikimbi
baada ya kubaini mtoto ana tatizo hili na sijui
aliko; mimi mwenyewe nashindwa kufanya
biashara yangu ya kutembeza mitumba
kwasababu hali ya mtoto huyu sio nzuri,”
alisema.
Alisema mtoto huyo huanguka na kupoteza
fahamu kwasababu ana tatizo lingine la
mtindio wa ubungo lililogundulika katika
hospitali ya Muhimbili.
Iwapo umeguswa na upo tayari kumsaidia
waweza kupiga namba 0754026299 ili
kuunganisha nguvu zetu.
Sunday, February 23, 2014
Mtoto wa ajabu azaliwa mkoani Iringa....Hafahamiki kama ni wa kiume au wa kike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment