MAMA wa majanga , Snura Antony Mushi kwa
mara ya kwanza amejitokeza hadharani na
kuzungumzia kauli ya msanii mwenzake wa
muziki wa mduara , Zuwena Yusuf Mohamed
‘Shilole ’ juu yake kuwa ameisha kimuziki
ndiyo maana ameamua kukimbilia muziki
wa Taarab .
Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole .
Akizungumza na mwandishi wetu hivi
karibuni , Snura ambaye anawika mitaani
kwa ngoma kali kama Majanga na
Nimevurugwa , alisema kitendo cha Shilole
‘kuponyokwa’ na maneno hayo ni ishara
tosha kuwa anamkubali na kufuatilia kazi
zake kwa ukaribu mkubwa.
Snura Antony Mushi .
“Sina tatizo na maneno ya Shilole , hiyo ni
ishara kuwa anafuatilia na kuzikubali sana
kazi zangu , wala hawezi kunizuia kufanya
kazi zangu kwa namna ambavyo nafikiria ,
yeye afanye yake, nami nishike ‘ hamsini
zangu ’, alisema Snura .
Thursday, February 20, 2014
SNURA AMBWATUKIA SHILOLE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hahahahaaa kaz ipoo
ReplyDeleteme nazan angekaa kmya apige kazi apate mafanikio amfunge mdomo mwenzake
ReplyDelete