Stori : Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya msanii anayekuja
kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za
Kibongo, Isabela Francis ‘ Vai wa Ukweli’
kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa
kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni
Fichua Maovu ‘OFM ’, ameibuka na kusema,
anajuta, amekoma na hatarudia tena .
Isabela Francis ‘ Vai wa Ukweli ’ akiwa katika
ofisi za GPL akiongea na OFM.
Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa
kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na
hili , Ijumaa toleo la wiki iliyopita, ambapo
msanii huyo aliingia mkenge baada ya
kukubali kukutana na ‘ pedeshee’ mmoja
kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda
kwa malipo ya shilingi 500, 000 .
Vai alivyonaswa akiwa mawindoni.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi ,
Jumatatu jijini Dar es Salaam , Vai alisema:
“Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana
lakini pia limenipa fundisho kubwa.
Nawaomba ndugu zangu na mashabiki wangu
wote wanisamehe kwa dhati kabisa.
Vai akificha sura yake baada ya kunaswa
na OFM .
“Naahidi sitarudia tena ujinga kama ule.
Ilikuwa ni tamaa tu. Hivi ninavyozungumza
na wewe nipo kwa editor (mhariri )
nasimamia editing (uhariri) ya filamu
yangu ambayo ipo katika hatua za mwisho
kuingia mitaani. Niko bize na kazi , acha
niwekeze kwenye ujasiriamali tu. Nawashauri
wasanii wenzangu tutulie maana OFM wapo
macho .”
.. .Akimsubiri pedeshee.
Alisema , katika filamu yake hiyo aliyoipa
jina la Beautiful Liar amewashirikisha
wakongwe Mohammed Fungafunga ‘ Jengua’ ,
Hashim Kambi ‘Wingo ’ na mastaa wengine
kwenye tasnia hiyo na kwamba mashabiki
wake wakae mkao wa kula.
.. .Baada ya mchezo kuharibika.
Kuomba msamaha ni uungwana , ikiwa Vai
umeona kosa lako na kuomba radhi ni
jambo zuri la kupongezwa . Tunakutakia kila
la heri katika mabadiliko hayo ,
tukikusisitiza iwe kweli maana OFM bado ipo
kazini. – MHARIRI .
Wednesday, February 26, 2014
VAI WA UKWELI: TAMAA YA FEDHA ILINIPONZA , NAJUTA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment