Wednesday, February 26, 2014

ABAMBWA AKIIBA KANISANI , AGEUZWA BUCHA !


Stori : Nyemo Chilongani na Deogratius
Mongela
KIOJA ! Kijana anayejulikana kwa jina
moja la Emmanuel ( 30 ), amejikuta
akipokea kipigo ‘hevi ’ baada ya kukamatwa
akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji
ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania ( KKKT) Usharika wa Kijitonyama,
Dar.
Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha
nguvu kutoka kwa wanachuo .
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani
hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo
ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara
kwa mara , alijikuta arobaini yake ikitimia
na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo
ambao kabla ya kuhoji zaidi , walimshushia
kipigo cha mbwa mwizi .
Wanachuo wakikagua baadhi ya vitu
alivyokutwa navyo Emmanuel .
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na
kanisani , kila siku watu wanalalamika
kuibiwa vitu vyao . Juzi tu, kuna watu
waliibiwa simu , wengine fedha lakini
hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia
hivyo, sasa huyu tutamkomesha , ” alisema
dada mmoja huku akiwa na furaha ya
kukamatwa kwa jamaa huyo .
Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo
wenye hasira .
Wanachuo hao, wakionekana kupania
kumfundisha adabu na kumwachisha
Emmanuel udokozi , walikuwa wakimhoji
maswali huku wakimwangushia kipigo
mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka
damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama
buchani .
Emmanuel akiwa na vitu vya wizi
alivyokutwa navyo .
Kama kawaida, mapaparazi wetu
hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu,
waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa
mali zao na mashuhuda waliomuona jamaa
huyo akiiba na kueleza mchezo mzima
ulivyokuwa .
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa ( alasiri)
nikaelekea mapokezi na baadaye darasani .
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama
ghafla , nikashtuka lakini sikutaka kuwa na
wasiwasi sana , nilidhani ni mwanachuo wa
hapa, ” alisema msichana mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na
kuendelea :
“Nikaondoka hapo na kupanda juu
(ghorofani ) . Moyo wangu ukawa mzito ,
ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na
kurudi kule mapokezi . Nilipofika mapokezi ,
yule mtu niliyemuona pale hakuwepo,
nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea
getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo
ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi ,
naye akaanza kukimbia mpaka
alipokamatwa, ” alisema Adolphina .
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa
nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule
ya sekondari ya mkoani Mbeya , cheti cha
kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine
vingi, vyote vikiwa si vyake .
Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za
mashine za ATM zikiwepo za CRDB , NMB na
NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa
anazitumia kwa ajili ya kuchukulia
‘mkwanja ’ kutoka katika akaunti za watu .
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake
alikutwa na simu aina ya Huawei yenye
thamani ya shilingi 360 , 000 na Nokia Asha
yenye thamani ya shilingi 150 , 000, ambazo
zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku
chache zilizopita .
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama –
Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo
mikononi mwa wanachuo hao ambapo
walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa
na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa
huyo akisulubiwa kwa hasira .

No comments:

Post a Comment

.