Wednesday, February 19, 2014

VICK KAMATA:UTAJIRI HUU UNAHITAJI MAELEZO YA ZIADA


WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi,
tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya
mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi
kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM),
Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na
utajiri balaa. Vicky amepata mafanikio
makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania
angependa kuyapata.
KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA Kabla
ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo
hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio
makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania
waliozaliwa katika familia duni. Katika
kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi
kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga
nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na
Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika
jamii. “Nimezaliwa kwenye familia duni,
nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na
muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya
msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika
harakati za kusaka maisha, baadaye
nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika
kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky
mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina
la baba halikutajwa).
MAFANIKIO YAANZA Mwaka 2006, Vicky
alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano. Mwaka
2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti
maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.
MJENGO WA GHOROFA MBILI Akiwa mbunge,
Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya
wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha
mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza
jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi
bilioni moja na milioni mia nne. Ndani ya
ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea
‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia
yake.
MAGARI YAKE SASA Kama walivyo matajiri
wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari
manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya
shilingi milioni 261. Ana Toyota Voxy- Noah
ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16.
Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na
thamani ya shilingi milioni 130. Mara nyingi
anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari
linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land
Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi
milioni 90. Pia mwanamama huyo ana gari aina
ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi
milioni 25.
ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU Wakati hayo
yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa,
mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu
Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya
mafanikio yake. “Vicky amenunua mgodi wa
dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu wa karibu,
hapendi kusema mafanikio yake wala watu
wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa,
muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema
chanzo cha habari.
ANA SHAMBA LA EKARI 157 Utajiri wa
mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa,
ni pamoja na shamba lenye ekari 150,
Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la
miti Kibamba, Dar lenye ekari 7. NI MFUGAJI
Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji
kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege
aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.
ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA Katika
mambo ambayo huenda yanachangia kuchota
baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya
sekondari watoto yatima, walemavu na
wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.
KIPATO CHAKE KIKOJE?
Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya
uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi
milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge,
ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.
AMFUNIKA ANNE MAKINDA Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba
la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la
bosi wake ambaye ni spika wa bunge,
mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake
ipo Kijitonyama.
ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME Uwazi
lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky
na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa
ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24. Ili
mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi
kwa dakika zisizopungua kumi.
HI NDIYO CCM INAYOWATETEA MASIKINI NA
WAKULIMA NAWANYONGE.

No comments:

Post a Comment

.