Wednesday, February 19, 2014

MCHAWI WA UNGO ADONDOKA, AGEUKA KUKU


HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za
kishirikina iligubika Jiji la Arusha kufuatia
mwanamke ambaye hakufahamika jina
kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya
Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika kuwa
kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo,
Uwazi limeona mengi.
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu
kando ya Barabara ya Arusha- Moshi
walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa
tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa
tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda,
Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku,
ghafla niliona kitu kipana kikidondokea
kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu
amekaa akiwa uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini
kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka,
badala yake mle mwenye ungo mkawa na kuku
mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa
sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na
nusu, ndipo wananchi hao wakaamua
kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua
na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo
kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na
petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata
na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio
hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa
Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa
maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo
alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP
Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana
kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya
maafande waliofika katika eneo hilo
walithibitisha.

No comments:

Post a Comment

.