Friday, January 3, 2014

EXCLUSIVE:- HATIMAYE SUPER STAR RAY C AFUNGUKA NA KUMCHANA LIVE JACKIE CLIFF SOMA ALICHOSEMA!!


Hivi karibuni aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva
na Radio presenter, mwana dada Rehema
Chalamila maarufu kwa jina la Ray C, aliingia
katika mjadala mkubwa na mashabiki wake
katika mtandao wa kijamii wa Instagram
baada ya kupost picha ya mrembo Jackie Cliff
aliyekamatwa nchini China kwa kosa la
kusafirisha madawa ya kulevya jijini Macau
nchini humo, na kutoa yake ya moyoni
kutokana na tukio hilo.
Post ya mwana dada Ray C ilizua mjadala
mkubwa katika mtandao wa huo wa Instagram
kiasi cha kwamba, fans wake walimpa support
kutokana na kauli yake ya kutaka Jackie
auwawe tu, huku fans wake wengine wakimsihi
asimuombe mabaya mrembo huyo aliyekamatwa.
Ray C alitoa kauli hiyo kutokana alishawahi
kuwa muathirika wa madawa hayo kipindi cha
nyuma na kusema kuwa watu wanaojihusisha na
biashara hiyo haramu hawana huruma kwa hiyo
na yeye hawaonei huruma hata kidogo kwa
sababu walimfanya ateseke yeye na familia
yake kipindi alipokuwa muathirika wa madawa
ya kulevya.

1 comment:

.