Friday, January 3, 2014

MKWASA , PONDAMALI, KUINOA YANGA


Uongozi wa Young Africans SC umepata
warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi
(Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali
na Dr . Suphian Juma ), huku wakiendelea na
mchakato kumpata kocha mkuu ambaye
atachukua nafasi ya mholanzi Ernie
Brandts aliyesitishiwa mkataba wake
mwishoni mwa mwaka 2013.
Charles Boniface Mkwasa 'Master ' aliyekua
kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting
katika mzunguko wa kwanza anachukua
nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred
Felix "Minziro " ambaye muda wake
umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013.
Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans
miaka ya 80 ' s kwa kiwango cha hali juu pia
alishawahi kuwa Kocha Mkuu/ Msaidizi kwa
kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti
jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni
katika mitaa ya Twiga na Jangwani .
Kocha wa makipa wa timu ya Taifa
Tanzania " Taifa Stars " Juma Pondamali
"Mensah " anachukua nafasi ya aliyekua
kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa
ambaye pia alistishiwa mkataba wake
mwishoni mwa mwaka 2013.
Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga
miaka ya 80 ' s kwa kwa kiwango cha hali ya
juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha
Tanzania kilichoshiriki mashindano ya
Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980,
sio mgeni katika timu ya Young Africans
kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi
kwa vipindi tofauti.
Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr
Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa
ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013
pamoja benchi la Ufundi.
Mara baada ya kuwapata viongozi hao
watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha Young
Africans kesho kitaanza mazoezi jioni
katika Uwanja wa Bora Kijitonyama
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
ya Vodacom pamoja na mashindano ya
Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza
benchi hilo la Ufundi mpaka
atakapopatikana kocha mkuu ambaye
watafanya watafanya kazi kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

.