Friday, January 3, 2014

MTANDAO WA UNGA WA JACK PATRICK UNATISHA


Jack akiwa chini ya ulinzi baada ya
kunaswa na dawa za kulevya China .
Na Mwandishi Wetu
BADO habari ya mjini ni skendo ya kunaswa
na madawa ya kulevya ‘ unga ’
inayomtafuna Video Queen wa Bongo,
Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘ Jack
Patrick ’ ambaye inadaiwa kuwa mtandao
wake wa biashara hiyo ni wa kutisha,
Ijumaa limetonywa .
Jack Patrick .
Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jack
ambaye aliomba chondechonde asitajwe ,
alidai kwa sasa vigogo wanaojihusisha na
biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha
kwa hofu kuwa modo huyo anaweza
kuwataja hivyo wanafanya kila
linalowezekana ili wamnusuru kama
ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘ Masogange’.
Ilisemekana kuwa katika mtandao huo,
vigogo hao wenye maskani jijini Dar,
Rwanda, Uganda , Kenya, Dubai , Thailand ,
Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha
kumuokoa Jack bila mafanikio .
“Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama
ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald )
aliyenaswa Sauz ( Afrika Kusini ) kwa sababu
wale ( China) Tanzania haikuwasaidia
kupata uhuru kama ilivyokuwa kwa Sauz .
Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za
kulevya alizokutwa nazo Jack Patrick .
“Ile ngoma ni mbichi , hakuna upenyo wa
rushwa pale . Ngojeni tusubiri hukumu
maana itakuwa kali sana , nazijua vizuri
sheria za China juu ya madawa ya
kulevya , ” alisema rafiki huyo wa Jack na
kuongeza:
“Hakuna ishu iliyoniuma kama ya Jack kwa
mwaka uliomalizika.”
Katika nusanusa za gazeti hili , ilidaiwa
kuwa bosi aliyemtuma Jack ni mwanamke
mmoja tajiri aishie jijini Dar ambaye ana
mtandao mkubwa wa biashara hiyo duniani.
Ili kuthibitisha kuwa mtandao uliodaiwa
kumtuma Jack unatisha na una watu
wazito , ilielezwa kwamba mrembo huyo
hakuwa peke yake kwani alifuatana na
warembo wawili, mmoja Mtanzania na
mwingine raia wa Rwanda ambao wao
walifanikiwa kuwatoroka polisi wa China.
Mbali na timu hiyo ya watu watatu
waliokuwa na mzigo mwilini, pia kulikuwa na
mtu mwingine aliyekuwa akiwasindikiza .
Ilidaiwa kuwa baada ya kupakia mzigo watu
hao waliondoka Dar kupitia Nairobi, Kenya
kisha Dubai ambapo walitua Bangkok,
Thailand kabla ya kutimkia Macau, Hong
Kong wakielekea Guangzhou , Mji Mkuu wa
Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Ilisemekana kuwa sehemu zote hizo
hawakushtukiwa kwa kuwa mtandao wao ni
mkubwa na inaonekana ni wazoefu kwa
shughuli hizo .
Kutisha kwingine kulikozungumziwa ni kiasi
cha mzigo aliokuwa amebeba Jack wa kilo
1 .1 za heroin wa zaidi ya Sh . milioni 200
kwa yeye peke yake bila kujua kiasi
walichokuwa wamepakia wenzake .
“Kinachoonekana jamaa wana mtandao
mkubwa maana ukicheki kiasi alichokutwa
nacho Jack ni kikubwa mno, ” alisema modo
maarufu anayefanya kazi za mitindo na
Jack .
Bado Jack yupo mikononi mwa polisi wa
China tangu aliponaswa kwenye Uwanja wa
Ndege wa Macau, China , Desemba 19 , mwaka
jana ambapo upelelezi wa awali
unaendelea.

No comments:

Post a Comment

.