MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye
jina lake halikupatikana mara moja
kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa
msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’
aitwaye Michael Sangu ‘Mike’ jambo
lililosababisha ale kichapo cha nguvu na
kuuanza mwaka mpya vibaya.
Tukio hilo lililovuta hisia za wengi, lilitokea siku
ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia
Jumatano, katika Ukumbi wa Mango Garden,
Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars
‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga
nyoyo za mashabiki wake.
KAMERA ZA IJUMAA
Paparazi wetu aliyekuwa ukumbini humo
alimuona Mike akiwa upande mwingine na
washikaji zake huku wakiendelea kula raha
wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati
mdada huyo ‘kibonge’ akiwa na mumewe na
watu wengine wakifanya yao.
Ijumaa lilipata shaka kidogo, baada ya
kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila
wimbo unapokolea na kwenda alipokuwa Mike
kisha kucheza naye.
Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema,
baada ya paparazi wetu kumshuhudia mume wa
dada huyo akionekana kumkaripia japo kwa
sauti ndogo mkewe kila aporudi akitokea
kucheza na Mike.
ONYO HALIKUZAA MATUNDA
Pamoja na onyo alilokuwa akitoa mume huyo
kwa mkewe mara kwa mara, bado dada huyo
alionekana kumfuata Mike na kucheza naye
tena kwa ukaribu kama vile wanajuana.
Baadaye jamaa huyo aliamua kuwashirikisha
marafiki aliokuwa amekaa nao meza moja
kuhusu tabia ya mkewe, wakamsihi asiende
tena kucheza lakini bado hakusikia.
“Sisi tulimwambia, mwenzako hataki uende
kucheza na yule msanii, anahisi labda kuna
kitu kinaendelea lakini hakusikia, sijui ni
pombe zilimzidi au vipi,” alisema mmoja wa
watu waliokuwa wameketi meza moja na
wanandoa hao muda mfupi baada ya tukio la
kichapo kutokea.
Akaongeza: “Kuna wakati alikuwa akijifanya
ameelewa, lakini sasa alikuwa akiaga na
kujifanya anakwenda msalani halafu mumewe
akifuatilia anagundua kumbe amemfuata Mike
ili wacheze, jamaa akachukia sana.”
KICHAPO
Baada ya mume kuona dharau za waziwazi
zikifanywa na mkewe mbele ya watu aliokuwa
amekaa nao, aliamua kusimama na kumfuata
alipokuwa akicheza na Mike.
Hakuwa na haja ya kuuliza chochote,
alimkamata mkewe na kuanza kumshushia
kichapo cha nguvu huku wengi wakiendelea
kuponda raha kama vile hakuna kilichotokea.
“Ni mke wake? Hizo ni dharau, acha apigwe.
Hawa wanawake wa Dar ni wajinga sana.
Utamwachaje mumeo uende kushobokea
wasanii? Huu ni upuuzi. Ni haki ale kichapo,”
alisikika akisema jamaa mmoja aliyekuwa
jirani na paparazi wetu.
DAMU CHAPACHAPA
Hasira zilipompanda yule jamaa, hakuchagua
mahali pa kupiga, alimvuta nywele na kumpiga
makonde kila sehemu ya mwili wake hali
iliyosababisha damu imwagike chapachapa
(angalia picha ukurasa wa mbele).
Mashuhuda walipoona damu imemwagika ndipo
wakaingiwa na huruma na kuamulia ugomvi
huo.
UTETEZI WA MKE
Katika kujitetea, mwanamke yule alimlaumu
mumewe kwa kumpiga hadi kufikia kutoa damu
kwa kosa la kucheza na Mike akisema kwamba,
haoni kosa lake.
“Mume wangu unanionea tu bure, huyu sina
uhusiano naye wowote ule... nacheza naye tu
kama marafiki. Simfahamu na wala sijawahi
kumuona zaidi ya kwenye filamu,” alisema
mwanamke huyo.
MIKE HUYU HAPA
Kwa upande wa Mike, alipoulizwa na mwandishi
wetu kuhusu kisanga hicho alisema,
anamshangaa jamaa mwenye mke kwa sababu
amemuonea mkewe bila sababu ya msingi.
“Kuna kosa gani watu kucheza muziki? Hapa ni
ukumbi wa muziki, tena usiku. Hakuna mipaka,
yeyote anaweza kucheza na yeyote. Ule mimi
naweza kusema ni ulimbukeni wa kutojua
mambo.
“Amemuonea... yule dada alikuwa anafurahi tu
sherehe za mwaka mpya ambapo staili yake ya
kucheza labda imemkera mumewe lakini kama
alikuwa hataki mkewe acheze na mtu mwingine,
si wangekaa tu chumbani kwao wawashe redio
wacheze wawili tu kuliko kuja kuleta kero
kwenye kumbi za burudani?” alisema Mike.
Alipoulizwa hajisikii vibaya kucheza na mke wa
mtu alijibu kwa kifupi sana: “Kwanza
ningejuaje?”
MADAI MENGINE
Ndoa ya Mike na Thea kwa sasa ipo kwenye
mgogoro mzito ambapo wawili hao wametengana
huku sababu kubwa ikitajwa na vyanzo vyetu
kuwa ni Thea kumtuhumu mumewe kuwa
hajatulia.
Bado tunafuatilia sakata hili, likikamilika
tutawaletea.
Friday, January 3, 2014
TIMBWILI LA KUFUNGULIA MWAKA..!! MKE ACHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME WA MSANII THEA..!! TAZAMA PICHA NA STORY KAMILI..!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hehehe chezea mke weyeee afu picha zingine wameungaa
ReplyDeletehahahahaha!!! kwi kwi kwi kwi teh teh teh teh aaaaaaaaah!!! mke naye alipenda kuktazwa kote hahaha
ReplyDelete