Monday, March 3, 2014

DIAMOND ANAVYOIBEBA TAITO YA SUKARI YA WAREMBO


WALIOSEMA ujana ni maji ya moto
hawakukosea. Mkali wao kwenye Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘ Diamond’ ni msanii
ambaye ana idadi kubwa ya msururu wa
wanawake ambao ametoka nao kimapenzi
ambapo , wapo wanaojulikana na wengine
hawajulikani.
Nasibu Abdul ‘ Diamond’.
Leo katika makala haya tunakuletea
wanawake ambao kwa nyakati tofauti
walibanjuka kimapenzi na Diamond ambao
kimsingi kutokana na idadi yake,
anadhihirisha jina lake la Sukari ya
Warembo
Takwimu zinaonesha kuwa karibu kila
mwaka jamaa anabadilisha wapenzi
ambapo wanawake wamekuwa wakipokezana
vijiti.
UPENDO MUSHI ‘PENDO ’
Huyu ni msanii wa filamu ambaye alitokea
katika Shindano la Maisha Plus. Aliwahi
kukiri kwamba alishatoka kimapenzi na
Diamond kabla hajawa maarufu kama
alivyo sasa, hawakudumu muda mrefu.
WEMA SEPETU
Ni mlimbwende wa Tanzania na msanii wa
filamu kwa sasa. Diamond baada ya kupata
umaarufu kidogo , alikutana na Wema na
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi jambo
lililofanya umaarufu wake kuzidi mara
dufu .
Wema na Diamond waliachana na kila
mmoja akawa anaendelea na maisha yake
lakini mwaka jana wawili hao walirudiana
na mpaka sasa wapo pamoja.
PENNIEL MUNGILWA ‘PENNY ’
Kwa muda huo ambao Diamond aliachana
na Wema , ulikuwa ni mwanya wa
Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penniel
Mungilwa kumiliki penzi la Mbongo Fleva
huyo .
Alikuwa ni rafiki wa karibu na Wema ,
akampindua kwa Diamond. Mapenzi yao
yalidumu kwa muda mfupi kabla ya mkali
huyo kurudisha majeshi kwa Wema kwa
mara nyingine.
ANGEL MAGGY
Diamond wakati akiwa na Wema kabla
hawajaachana iliripotiwa kwamba alikuwa
akisaliti penzi lao ambapo alitoka
kimapenzi na msichana Angel ambaye ni
Mkenya lakini hawakukaa muda mrefu,
wakamwagana .
JOKATE MWEGELO
Ni mwanamitindo maarufu Tanzania. Penzi
lao lilikuwa la muda mfupi na la siri kwani
hawakujiachia kama ilivyokuwa kwa Penny
na Wema . Huyu naye alikuwa ni rafiki wa
Wema lakini alitoka naye kimapenzi
ambapo baada ya kuachana , Diamond
alimuomba msamaha na kusema alimkosea
sana kwani ni mwanamke ambaye
alimpenda lakini alimpotezea baada ya
kumpata Wema .
JACQUELINE WOLPER
Ni msanii wa filamu Bongo. Wolper na
Diamond walitoka kimapenzi lakini
waliachana katika mazingira ya
kutatanisha jambo lililomfanya Diamond
amtungie wimbo kutokana na jinsi
alivyoumia .
NAIMA
Huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa
Wema lakini alitoka kimapenzi na Diamond
hali iliyosababisha wanawake hawa kuwa na
bifu kwa sababu ya kushea mwanaume huyo
mmoja .
REHEMA FABIAN
Huyu ni mrembo aliyeshikilia Taji la Miss
Kiswahili ambapo naye aliingia kwenye listi
ya kutoka kimapenzi na Diamond. Uhusiano
wa wawili hawa haukuwa wa muda mrefu
ilikuwa ni kama kupita tu.
NATASHA
Ni mwanadada aliyeshiriki kwenye moja ya
video za Diamond. Baada ya hapo habari
zilienea kwamba Diamond amempitia
ambapo nao hawakukaa muda mrefu.
Baada ya sarakasi zote za wapenzi, sasa
Diamond ametulia kwa Beautiful Onyinye ,
Wema Sepetu ! Tutegemee nini ? Yetu macho .

No comments:

Post a Comment

.