Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia alikuwa
ametuma salamu za kumtakia ushindi Lupita
Mcheza sinema maarufu Lupita Nyong’o ambaye
ni raia wa Kenya, Jumapili ameshinda tuzo la
kifahari la Oscar huko Hollywood California.
Lupita alipata tuzo hilo kwa kuwa muigizaji
msaidizi bora zaidi kwenye filamu iitwayo“12
years A Slave”.
Baada ya kupokea tuzo hilo, Lupita alitoa
hotuba yenye hisia kali na kuwashukuru wote
waliomwezesha kushinda tuzo hilo la Oscar.
Awali macho ya dunia kwa wapenzi wa filam
yalielekezwa huko Hollywood kutizama tuzo za
mwaka wa 86 za Oscar zikitunukiwa wasanii
mbali mbali wa filam duniani.
Kwa upande wa Afrika mcheza filamu mwingine
wa mara ya kwanza Barkhad Abdi ambaye ni
raia wa Somalia aliteuliwa kuwania katika
nafasi ya waigizaji wasaidizi ambapo alishiriki
katika filamu “Captain Phillips” ambapo
muigizaji Jared Leto alipata ushindi.
Vyombo vya habari vya Kenya viliripoti kuwa
wakenya na waafrika kwa jumla walikuwa
wakisubiri kuona ikiwa muigizaji Lupita Nyong’o
atapata tuzo hilo. Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta pia alikuwa ametuma salamu za
kumtakia ushindi Lupita ,katika ujumbe kwenye
ukurasa wake wa Facebook.
Sunday, March 2, 2014
LUPITA NYON’GO AANDIKA HISTORIA BARANI AFRIKA NA KUNYAKUWA OSCAR.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment