RAIS wa Shirikisho la Tanzania ( TFF), Jamal
Malinzi ameunda kamati ya watu tisa
kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu
TFF ilipojiunga na Shirikisho la Soka la
Kimataifa ( Fifa ) .
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni Miss
Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu .
TFF ilipata uanachama waFifa , Oktoba 8 ,
1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50
kwa kufanya shughuli mbalimbali za soka.
Kamati hiyo itaongozwa na mhariri
mtendaji wa kampuni ya magazeti ya
serikali, Gabriel Nderumaki wakati katibu
atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti
wa Chama cha Soka cha Wanawake (TWFA ).
Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu ,
Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba , Richard
Kasesela, Boniface Wambura na Meneja
Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa
hivi karibuni .
Kamati itafanya kikao chake cha kwanza
Jumatatu ( Machi 3 , 2014) kwenye hoteli ya
Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7
mchana.
Saturday, March 1, 2014
Malinzi amteua Miss Tanzania kamati ya miaka 50 Fifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment