KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, juzi
Alhamisi warembo kibao walijikuta
wakimiminika kwenye mazoezi ya Yanga kwa
ajili ya kuwashuhudia nyota wa kikosi hicho ,
Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi kwenye
Uwanja wa Boko Veterani uliopo Boko jijini
Dar.
Yanga ipo kwenye maandalizi makali ya
mechi dhidi ya Al Ahly ya Misri , ukiwa ni
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
utakaopigwa kesho Jumamosi.
Akizungumza na Championi Jumamosi ,
mmoja kati ya warembo hao waliojitokeza
aliyefahamika kwa jina la Asha Said,
alisema aliamua kuacha kazi zake
nyumbani kwa ajili ya kwenda
kuwashuhudia nyota hao ambao amekuwa
akiwakubali kwa namna wanavyofanya kazi
zao.
“Nimeona bora leo nije mwenyewe
kuwashuhudia kwa macho yangu , kwani kila
siku ninawaona kwenye runinga tu na
kuwasikia redioni , sikuwahi kuwaona ‘ live ’,
nashukuru leo nimewashuhudia mwenyewe
na nimebahatika kupiga nao picha .
“Nawaombea washinde katika mechi yao
dhidi ya hao Warabu kwani Yanga ndiyo
timu pekee iliyobakia kuiwakilisha nchi yetu
katika mashindano ya kimataifa kwa ngazi
ya klabu , ” alisema Asha .
Katika mazoezi hayo, akina dada na akina
mama walionekana kwa wingi uwanjani hapo
licha ya fikra za watu wengi kudhania kuwa
mchezo wa soka ni wa wanaume pekee .
Malinzi amteua Miss Tanzania kamati ya
miaka 50 Fifa
Saturday, March 1, 2014
Okwi , Ngassa wajaza warembo mazoezini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment