Omary Mdose na Said Ally
KUELEKEA kwenye mechi kali ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly
ya Misri , Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ,
Masau Bwire amesema wawakilishi hao
wasidhani Al Ahly ni kama Komorozine .
Yanga ambayo iliitoa Komorozine kwa mabao
12- 2 , sasa inakutana na Al Ahly, leo
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika .
Akizungumza na Championi Ijumaa , Bwire
alisema endapo Yanga wakitaka kuibuka na
ushindi katika mchezo huo, basi lazima
wafanye kazi ya ziada na kuacha kucheza
kwa staili waliyoitumia dhidi ya Ruvu na
kupata ushindi wa mabao 7 - 0 .
“Wasibweteke na ushindi walioupata
walipocheza na sisi pamoja na wale
Wacomoro, watambue kuwa Waarabu ni
wabaya sana wakiwa nyumbani au ugenini
na hata wakifungwa basi huwa ni mabao
machache sana , ” alisema Bwire.
Saturday, March 1, 2014
Masau amwaga shombo tena kwa Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment