Saturday, March 1, 2014

Zahoro Pazi apewa siku 14 Simba SC


Na Hans Mloli
KIUNGO mshambuliaji wa Simba , Zahoro
Pazi , atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa
muda wa wiki mbili ambazo ni sawa na siku
14 kutokana na majeraha ya mishipa ya
enka .
Zahor alidondoka na kuumia alipokuwa
kwenye harakati za kuuzuia mpira mrefu
uliokuwa unakwenda nje Jumatano iliyopita
wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar.
Akizungumza na Championi Jumamosi , Ofisa
Habari wa Simba , Asha Muhaji alisema
kwamba Zahoro amefungwa bendeji ngumu
itakayosaidia mishipa ya enka kupona
mapema zaidi .
“Kuna mishipa ya enka inamsumbua hivyo
amefungwa hogo, kisha baada ya hizo wiki
mbili atatolewa na atarudishwa hospitali
kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusu
maumivu hayo, ” alisema Muhaji.

No comments:

Post a Comment

.