Saturday, March 1, 2014

YANGA CHINJACHINJA


YANGA inashuka kwenye Uwanja wa Taifa
kuivaa Al Ahly leo ambapo upinzani
unatarajiwa kuwa mkubwa, lakini neno
moja ambalo mashabiki wa Yanga wanataka
waone likitimia ni ‘ kuwachinja’ wapinzani
wao hao .
Mechi hiyo ya raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Afrika ni ya kwanza na
inatarajiwa kuwa ya upinzani mkali kwa
kuwa Al Ahly ndiyo mabingwa watetezi wa
ligi hiyo , pia kumekuwa na vitu vingi
vimetokea kabla ya kupulizwa kwa kipenga
cha kuanzisha mchezo baina ya timu hizo :
Al Ahly wagoma kuzungumzia mchezo :
Kama ilivyo kawaida ya wawakilishi wa
benchi la ufundi kuuzungumzia mchezo
kabla, Al Ahly waligoma bila kutoa sababu
za msingi .
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) Boniface Wambura , aliliambia gazeti
hili kuwa Al Ahly walifikishiwa taarifa za
kuzungumza kwenye mkutano na
wanahabari, lakini wakagoma .
“Wametoa sababu kuwa siyo lazima kisheria ,
basi hatuwezi kuwalazimisha labda baada
ya mechi hapo lazima waongee. Ni sheria, ”
alisema Wambura .
Wanavyosema wadau Yanga Vs Al Ahly:
Jamal Malinzi (Rais TFF) : “ Nilipokuwa
naangalia fainali za Super Cup niliambiwa
Al Ahly haifanyi vizuri nyumbani,
imefungwa mechi tatu , hivyo wachezaji wetu
hawatakiwi kuiogopa .
“Tunajua wana fitna sana hasa wakiwa
kwao , wachezaji wanatakiwa wanapokwenda
Misri wasiangalie wala kuogopa baruti,
fataki, filimbi feki na badala yake walenge
mpira wao .”
Fred Minziro ( Kocha JKT Ruvu) : “ Wachezaji
wanatakiwa kupigana kufa au kupona ili
kuwafunga Al Ahly nyumbani .”
Choke Abeid ( Kocha JKT Oljoro) : “ Mechi ni
dakika 90 na timu zote zina maprofesheno ,
hakuna sababu ya Yanga kuhofia kwani ina
wachezaji wa kimataifa .”
Madaraka Suleiman (straika wa zamani
Simba ) : “ Yanga wajitahidi washinde mabao
zaidi ya mawili , kama ni fitna wafanye
hapa, wasisubiri baadaye , kwa kuongea na
waamuzi .”
Juma Mwambusi ( Kocha Mbeya City ): “Yanga
inatakiwa ijipange , ushindi wa nyumbani ni
muhimu .”
Yusufu Chipo (Kocha Coastal ) : “ Mechi
itakuwa ngumu , Yanga watumie vizuri
uwanja wa nyumbani .”
Zamoyoni Mogella (straika wa zamani
Simba ) : “ Unaweza kusema sana na
waandishi wakaandika lakini mwisho wa
siku wenye maamuzi ni wachezaji wa Yanga
wenyewe. ”
Aboutrika abadili mfumo Yanga:
Kocha Mkuu wa Yanga , Mholanzi Hans van
Der Pluijm , ameshaandaa mikakati , mbinu
na mifumo mbalimbali ya kuisambaratisha
Al Ahly lakini akakiri kama kiungo
Mohammed Aboutrika angekuwemo kwenye
kikosi kilichotua nchini basi mfumo wa
Yanga ungebadilika .
Aboutrika alistaafu soka mwaka jana hivyo
atakosekana kwenye michuano ya mwaka
huu. Pluijm amesema wakati Aboutrika yupo
Al Ahly timu hiyo ilikuwa ikitumia zaidi
sehemu ya kiungo kutengeneza nafasi za
kufunga , lakini tangu ameondoka
wanaotumika sasa ni mawinga.

No comments:

Post a Comment

.