Stori : Sifael Paul
Lile sakata la kukamatwa kwa yule mganga
wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz ’, Ustadh Yahya kwa
msala wa wizi wa gari , limechukua sura
mpya baada ya mke wa mwenye gari , Edric
Magayane kuibuka na kufunguka mazito.
Mganga wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz ’, Ustadh Yahya.
Akizungumza na gazeti hili , mke huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Emida Denson
alisema kuwa gari hilo aina ya Toyota Rav4
lilikuwa mali ya familia kabla ya mumewe
kudai lilipata ajali hivyo lipo gereji.
Alisema kuwa baadaye mumewe alidai kuwa
aliliuza akaongezea fedha kisha akanunua
lingine aina ya Toyota Prado .
Alisema habari kuwa gari hilo liliibwa
maeneo ya Kariakoo - Msimbazi, Dar
hazikuwa za kweli kwani ukweli ni kwamba
mumewe huyo alikuwa amemhonga
mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la
Mwanahamis.
“Huyo Mwanahamis amenisababishia mateso
makubwa kwenye ndoa yangu karibia miaka
miwili sasa. Yaani ndoa yangu ni sarakasi
tupu kwa sababu yake.
Edric Magayane na mkewe Emida Denson .
“Ukweli ni kwamba baada ya kuhongwa lile
gari alikuwa hajui kuliendesha .
Alichokifanya akamwachia Ustadh. Hayo
mengine ya kushirikiana juu ya biashara
zao za uganga hayanihusu.
“Sasa basi baada ya kuona gari liko
mikononi mwa Ustadh ndipo mume wangu
akalitaka ndiyo maana wamefikia hapo.
“Kinachoniuma ni kwamba mbali na gari ,
mume wangu alifikia hatua ya kuja
kumpangishia Mwanahamis jirani na
nyumba yetu maeneo ya Machimbo -Mwisho
wa Lami ( Yombo jijini Dar)
“Mbaya zaidi watu wakawa wanamuona
mume wangu akiingia kwa Mwanahamis,
nimedhalilika sana .
“Nalea watoto wanne peke yangu , wakwangu
wawili na wawili wa mume wangu kwa
mwanamke mwingine .
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ .
“Baada ya kuona ndoa inanitesa
nilikwenda kwa mchungaji Kimaro
aliyefungisha ndoa yetu kwenye Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ),
Usharika wa Kariakoo nikamweleza mateso
ninayopata.
“Alituita wote, akasemwa lakini baada ya
hapo manyanyaso yakaendelea japo
walihamia Banana- Ukonga ndiko
wanakoishi hadi leo .
“Pia nilikwenda kwenye Dawati la Jinsia
wilayani Temeke na baadaye Ustawi wa
Jamii .
“Huko kote ilishindikana na sasa bora anipe
talaka yangu tugawane mali kwa sababu
nilipokutana naye hakuwa na kitu chochote,
tulikuwa tukilala chini , ” alisema mwanamke
huyo kwa uchungu huku akitoa cheti cha
ndoa ( nakala ipo).
Kwa upande wake mume wa mwanamke
alipotafutwa na kusomewa mlolongo wa
sarakasi alizozieleza mkewe, alisema kuwa
gari hilo lilikuwa mali yake na kwamba
lilipata ajali likakaa gereji muda mrefu na
lilipopona alikuwa akilitumia mwenyewe .
Kuhusu kuwa na hawara Mwanahamis ,
jamaa huyo alidai kwamba aliamua kuwa
na mwanamke huyo kwa kuwa mkewe
alikuwa ana matatizo ambayo hata hivyo
hakutaka kuyaainisha .
“Naishi naye ( mkewe) lakini kila mtu na
chumba chake , huyo mwanamke ana
matatizo yake ndiyo maana nikatafuta mtu
mwingine, hizo habari anazolalamika,
anazusha tu, nimempa uhuru aniache na
wangu na yeye atafute mwanaume
mwingine, ” alisema mwanaume huyo .
Kuhusu gari analodaiwa kukutwa nalo
mganga wa Diamond, habari zilieleza kuwa
Ustadh aliachiwa kwa dhamana na bado
gari hilo lipo mikononi mwa polisi likisubiri
kesi kwenda mahakamani.
Saturday, March 1, 2014
SAKATA LA MGAGA WA DIAMOND: MKE WA MWENYE GARI LILILOIBWA AIBUKA, AFUNGUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment