Mshindi wa tuzo tano za muziki za Kilimanjaro
2011, Abbas Kinzasa ‘Twenty Percent’
amesema ameamua kurudi kwa prodicer wake
John Shariza, maarufu kwa jina la Man Walter
ili kuwaburudisha mashabiki ambao wanahisi
kuna kitu wanakosa.
20% ameiambia Bongo5 kuwa kuungana tena
na Man Walter ni kwaajili ya kuwarudisha
mashabiki ambao imani zao zinawapa 20% na
Man Walter kutokuwa pamoja zinasababisha
mashabiki wa muziki kukosa burudani.
“Tumerudi ili mradi kuweka sawa mambo watu
wataanza kufurahia ile combination ya
ukweli,ingawa bado hatuna mkataba ni kama
tunafanya kazi hasa kazi tu.Kutokana ni muda
mrefu umepita kuna ngoma inakuja inaitwa
‘Subira yavuta heri’kwahiyo baada ya hapo
wataendelea kupata ngoma nyingine zaidi
kutoka kwa Man Walter na 20%,” alisema.
“Kwa upande wa filamu wasubiri filamu mwezi
wa kwanza inatoka inaitwa ‘Lazima ajitambue
kwanini haujitambui’ ambayo izungumzia
mazingira ya maisha na muziki kama
ilivyokuwa filamu yangu ya kwanza. Filamu
yangu ya kwanza imenifanya niweze kuongeza
mashabiki, imefanya watu waamini naweza
kufanya vitu vingi na vyote vipo kwenye damu
ndiyo maana ninafanya vizuri,” aliongeza
msanii huyo.
“Mimi na Man Walter tuna fanana,kwasababu
nasema Man Walter anakipaji na mimi nina
kipaji lakini vipaji vyetu lazima vivaane
tunaweza kutoa kitu kimoja.Katika kipindi
ambacho mimi na Man Walter tumekosana n
ikipindi ambacho Man Walter anapigiwa kelele
za kushangiliwa na mimi napigiwa kelele za
kushangiliwa yaani kwamba ni mastaa.
Ni wakati ambao ni mgumu sana kwa mtu
ambaye anashika ile nafasi yaani ni staa,
unaweza ukapotea njia unaweza
ukafanyaje.Lakini wewe huwezi kuliona hilo ila
yule mtu ambaye amekaa pembeni kama
mkumbwa wako,pengine alivutiwa na kazi
zako, basi akawa anaangalia maendeleo yako
ya kazi hataki upotee, hataki uteleze. Kwahiyo
anaangaliwa pale ambapo uliteleza, wapi
ambapo pakirekebishika wewe unaweza kurudi
katika hali yako ambayo inatakiwa uwe.
Ndio watu ambao walikaa wakaona kuna
uhumimu wakutii hizi kiu za wanajamii ambao
wanawazunguka Man Walter na 20%, na je?
20% na Man Walter kuna nini kinawazunguka
mpaka wakose maziwa,wakose maji,wakose
juice? Kuna watu ambao wana hekima zao,
mimi naita wenye busara zao wakakaa chini
wakasema kuna kila sababu za hawa watu,
kukaa pamoja na kufanya kazi. Sasa mtindo
wa kazi ndio kitu ambacho kinatakiwa kukaa
chini,aina gani ya kazi ni milolongo gani ya
kazi ,jinsi kazi itakavyokwenda bila
kusumbuana. Maybe wameona wapi
tulipokosea ndio maana kila kitu kinaenda kwa
process.”
Monday, December 9, 2013
20 Percent azungumzia mipango mikubwa baada ya kupatana tena na Man Walter
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Money money ilisababiisha nikutoroke
ReplyDeleteHahahaha sa kijana alikua anapapalika nini tuzo zilimchanganya
ReplyDelete