Wednesday, December 4, 2013

AIBU...!! TAJIRI ASABABISHA TIMBWILI LA KUFA MTU BAADA YA KUGONGANISHA WANAWAKE UWANJA WA NDEGE DAR..!!


MWANAUME mmoja aliyeelezwa kuwa ni tajiri
mwenye nazo mjini, amezua tafrani na
kusababisha timbwili la nguvu kwa dakika
kadhaa baada ya kugonganisha wanawake
wawili waliodaiwa kuwa chini ya miliki yake kwa
wakati mmoja, subiri hapohapo tukujuze!
Mtiti huo uliovuta hisia za wengi ulichukua
nafasi Ijumaa iliyopita, mishale ya saa sita na
dakika zake usiku, pande za Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’ ambapo
mwanaume huyo ambaye jina lake
halikupatikana mara moja alitua na Ndege ya
Shirika la Kenya.
ANGALIA SINEMA
Hali ya hewa ilikuwa ya kuridhisha kabisa katika
eneo la uwanja wa ndege wakati paparazi wetu
akiwa kwenye sehemu maalum ya kusubiria
abiria wanaotua uwanjani hapo wakitokea nje ya
nchi.
Paparazi wetu alikuwa akimsubiri mgeni wake
lakini kama ilivyo kawaida ya wanakikosi cha
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ alikuwa na zana
zake za kazi kama kawaida.
Wakati wageni wakianza kutoka, ghafla zilisikika
kelele pembeni mwa sehemu aliyokuwa paparazi
wetu, akajiuliza kunani? Akaweka zana zake za
kazi sawa kisha akajongea eneo la tukio.
VARANGATI LA NGUVU
Kamera za Risasi Mchanganyiko zilishuhudia
wanawake wawili wakikunjana na kupigana
makonde huku mmoja akimshutumu mwenzake
kumwibia mumewe (haikujulikana kama ni wa
ndoa). Alisema: “Wewe mpumbavu mwizi wa
waume za watu, nitakukomesha leo. Si umezoea
kuiba waume za watu? Sasa utanijua mimi ni
nani?”
Mwanamke huyo aliyeonekana kuwa na jazba,
alikuwa na watoto wake wawili waliovalia sare
za shule ambao walikuwa wakimvuta na kumsihi
aachane na ugomvi.
MSHANGAO NI HUU!
Sekeseke wakati likiendelea, yule mwanamke
ambaye alikuwa akidai kuibiwa mumewe kwa
muda mrefu na mwanamke huyo, watoto wake
wawili walikuwa naye sambamba huku wakijaribu
kumtuliza ingawa kiumri ni wadogo.
Mwanamke aliyedaiwa kuchukua mume wa
mwenzake naye alikuwa na mtoto wake mmoja
ambaye alikuwa akimvuta akitaka kumtoa
mikononi mwa mwanamke aliyedaiwa kuwa
mmiliki rasmi wa tajiri huyo.
Mshangao mkubwa ni kitendo cha watoto hao
wote kuwa wamevaa sare za shule, tena
zikionekana kuwa za shule moja – maswali
yalikuwa mengi kuliko majibu!
“Hawa watoto sijui wamekuja na huyu jamaa?
Maana wanaonekana kama wanasoma shule
moja na wapo na vifaa vyao vyote vya shule.
Hapa hata haileweki jamani,” alisikika dereva
teksi mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.
MAELEZO MENGINE
Mashuhuda walisema, awali tajiri yule wakati
anatoka katika sehemu maalum ya abiria
wanaoingia nchini, alikimbiliwa na mwanamke
yule anayedaiwa kuwa kimada na kumpokea
kisha kumbusu na kumpa pole kwa safari.
“Tatizo lilianzia pale yule mwanamke
mwembamba mwenye nguo nyekundu alipoenda
kumpokea jamaa. Alimfuata na kumkumbatia
kisha akambusu, basi hapo tafrani ikatokea. Yule
mke wa jamaa alikwenda haraka na kumvamia
kisha kuanza kumpiga,” alisikika mmoja wa
mashuhuda hao.
TAJIRI AWAZODOA WALIOMSHANGAA!
Wakati tafrani ile ikiendelea, mwanaume huyo
aliwaingilia kati na kuwaamulia, jambo
lililozidisha watazamaji wa sinema hiyo ya bure
kushangaa.
Katika hali ya kushangaza, tajiri huyo aliwananga
watu waliokuwa wakimshangaa akisema: “Sasa
kipi cha ajabu? Ni mwanaume gani hapa ambaye
hajawahi kufumaniwa? Haya ni mambo ya
kawaida, endeleeni na shughuli zenu nitamaliza
hii ishu mwenyewe.”
Juhudi za tajiri huyo kuwaachanisha zilizaa
matunda, kwani zaidi ya kutumia nguvu,
alionesha ‘uanaume’ wake kwa wanawake hao
ambao walikubali kuachana na ugomvi huo
ingawa kila mmoja alionekana kuwa na hasira na
mwenzake.
Baadaye yule mwanamke aliyedaiwa kuwa ndiye
mke halali wa tajiri yule, aliondoka naye wakiwa
na watoto wao wawili, mwingine akaondoka na
mtoto wake.

No comments:

Post a Comment

.