Hii ni aibu kwa taifa! ‘Makachero’ wa Oparesheni
Fichua Maovu (OFM) iliyo chini ya Global
Publishers wameibua uozo mwingine jijini
Mwanza baada ya kubamba tukio la kusikitisha
na kufedhehesha la mtoto mwenye umri wa
miaka 12 akijiuza.
Uchunguzi wa OFM jijini hapa wiki iliyopita
umebaini kuwa vitendo hivyo vinaonekana vya
kawaida na kuzoeleka miongoni mwa wakazi
wake, jambo linalotia dosari kwa mji huo
unaosifika kwa usafi wa hali ya juu wa
mazingira.
OFM ilishuhudia wimbi kubwa la watoto wa kike
walio chini ya umri wa miaka 18 wakijihusisha
na biashara haramu ya kuuza miili nyakati za
usiku.
Awali taarifa za uwepo wa watoto hao jijini
Mwanza zilipokelewa katika ofisi za Global
Publishers jijini Dar kutoka kwa baadhi ya
wasafiri na wakazi wa jiji hilo wakiomba
kupelekwa kwa OFM kutokana na suala hilo
kutofanyiwa ufumbuzi na taasisi husika.
“Jamani hii ni aibu kwa taifa letu! Hapa Mwanza
mjini kuna vibinti vidogo sana vinauza miili,
tunaomba OFM isibakie Dar pekee, njooni na
huku hali inatisha,” aliomba mkazi mmoja wa
Mwanza.
OFM huwa haipuuzi taarifa kutoka kwa vyanzo
vyake hivyo iling’oa nanga katika jiji la maraha
na karaha la Dar na kutinga rasmi Jiji la Miamba
(Rocky City) Mwanza kufanyia kazi
kilichosemwa.
Kweli watoa taarifa walikuwa na hoja kwani
katika viunga vya Mwanza Mjini maeneo ya
Kauma jirani na Mnara wa Samaki kwenye
Barabara ya Nyerere, OFM iliwashuhudia watoto
hao wakijiuza bila wasiwasi huku wakilindwa na
watoto wenzao wa jinsia ya kiume waliokuwa na
chupa na viwembe kama silaha zao.
Katika utafiti wake, mmoja wa ‘makamanda’ wa
OFM alijifanya mteja kwa watoto hao ambapo
alifanikiwa kuongea nao.
Kuhusu bei, mmoja alieleza kuwa huwa
wanatoza shilingi 20,000 kwa kulala usiku
mzima na elfu 5,000 kwa short time.
Maskini! Mtoto Aisha (12) alikuwa yupo tayari
kuchukuliwa kwa makubaliano yoyote ambapo
alisema kinachomfanya kujihusisha na biashara
hiyo ni hali ngumu ya maisha na wazazi wake
kushindwa kumsomesha.
Katika kazi hiyo ya OFM jijini Mwanza, mtoto
huyo alidai kuwa alipopelekwa shule ya msingi
huko wilayani Sengerema, wazazi wake
walishindwa kumudu michango ya kila kukicha
hivyo akabaki nyumbani hadi alipotorokea jijini.
Akizungumza na OFM juu ya sakati hilo la
kushamiri kwa biashara hiyo haramu, Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema: “Sina
taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao
wanaojiuza ndiyo nasikia labda nipate muda wa
kuzungumza na uongozi wa chini nitalichukulia
hatua mara moja.”
Imeandikwa na Chande Abdallah na Denis
Mtima waliokuwa Mwanza.
Wednesday, December 4, 2013
NI UGUMU WA MAISHA AU NINI?? MTOTO WA MIAKA 12 ABAMBWA AKIJIUZA KAMA WANAVYOJIUZA WENGINE...!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment