Friday, December 13, 2013

Aliyejihakikishia namba Simba ni mmoja tu


Na Nicodemus Jonas
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic
‘ Loga ’ amesema mpaka kufikia sasa wakati
timu yake ikiendelea kujifua , mchezaji
anayemuona kuwa na uhakika wa namba
kwenye safu ya ushambuliaji ni Uhuru
Selemani.
Uhuru ambaye amerejea klabuni hapo baada
ya kuichezea Coastal Union kwa mkopo ,
amekuwa akionyesha kiwango kizuri na
kujituma katika mazoezi .
“Uhuru ni mchezaji mzuri uwanjani, ndiye
naona ana uhakika wa namba kwenye
ushambuliaji, labda sijui hapo baadaye kama
atakuja kubadilika , lakini mpaka sasa ndiye
anaona ananifaa mbele , ” alisema Loga .
Uhuru alipelekwa Azam FC kwa mkopo kisha
Coastal lakini kote alikuwa na wakati mgumu
wa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza

No comments:

Post a Comment

.