Kikosi cha JKT Oljoro .
Na Amisa Mmbaga
KOCHA wa JKT Oljoro , Hemed Morocco ,
amesema atahakikisha anakipika vilivyo
kikosi chake na kuwa tishio kwenye
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Morocco amejiunga na Oljoro kwa mkataba
wa mwaka mmoja mara baada ya ajira yake
katika timu ya Coastal Union kufikia tamati
hivi karibuni .
Morocco ambaye ameanza majukumu mapya
katika timu hiyo inayoshika nafasi ya 11
kwenye msimamo wa ligi , amesema vijana
wake wapo vizuri na maandalizi yanaendelea
na hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi
mpaka sasa .
“Wachezaji wapo vizuri kwani nimekaa nao
kwa muda wa wiki mbili sasa japo sijawajua
vizuri wachezaji wote lakini wanaonyesha
muelekeo mzuri na naamini watafanya vizuri.
“Natarajia kukibadilisha kikosi kwa lengo la
kufanya vizuri zaidi kwani tulifanya vibaya
katika mzunguko wa kwanza , ” alisema
Morocco ambaye timu yake ina pointi 10
katika mechi 13 .
Friday, December 13, 2013
Morocco atamba kuipaisha Oljoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment