Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi .
Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi
amemaliza majaribio yake ya wiki moja
aliyokwenda kufanya nchini Malaysia katika
Klabu za Teregganu na T- Team ambapo
amerejea nchini .
Bahanuzi aliondoka nchini Alhamisi iliyopita
kuelekea nchini humo kwenda kufanya
majaribio ya wiki moja kwa ajili ya kucheza
soka la kulipwa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Msemaji
wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema Bahanuzi
alifanya majaribio katika timu mbili tofauti
alipokuwa Malaysia katika timu za Teregganu
na T - Team .
“Bahanuzi amemaliza leo ( Jumatano )
majaribio na usiku ataanza safari ya kurudi
Tanzania kwa ajili ya kujiunga na wenzake
mara baada ya kuwasili. Timu zote hizo zipo
nchini Malaysia zinashiriki Super League
lakini majibu ya majaribio bado sijayapata ,”
alisema Baraka .
Friday, December 13, 2013
Bahanuzi arudi Bongo kama alivyoondoka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment