Friday, December 13, 2013

AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA KUUNGUA VIBAYA KISA MAPENZI HUKO ARUSHA.


TAHADHARI KWA PICHA UTAKAZOZIONA
Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo
akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti
aliyemwagiwa maji ya moto mwili
mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano
na mume wa mtu.
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya
moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa
na uhusiano na mume wa mtu.
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya
moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa
na uhusiano na mume wa mtu.
Na Gadiola Emanuel -Arusha
Mwanamke mmoja mkazi wa
Mbuguni Arusha, Bi. Neema Teti
amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji ya moto katika
sehemu mbalimbali za mwili wake
katika kisa kinachodaiwa kuwa ni
wivu wa mapenzi. Tukio hilo
limetokea baada ya mtekelezaji wa
kitendo hicho Mama Tatu Msuya
ambaye ni jirani yake akidaiwa
kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mume
wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi
hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount
Meru alikolazwa, Neema ameelezea
tukio hilo kuwa limetokea juma
lililopita baada ya kuitikia mwito wa
jirani yake Tatu Msuya uliomtaka
afike nyumbani kwake kwaajili ya
kumsaidia uangalizi wa familia yake
kutokana na kuhitajika msibani na
ndipo alipomjeruhi vibaya kwa
kumwagia maji ya moto.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya
Mount Meru,N eema Bayo amesema
majeruhi huyo aliletwa hospitalini
hapo akiwa katika hali mbaya lakini
hali yake imezidi kuimarika baada
ya kupatiwa matibabu na jopo la
madaktari hospitalini hapo. Nae
Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount
Meru Hospitali Bi.Neema Bayo
amesema matukio kama hayo
yakizidi kushamiri katika maeneo
mbalimbali nchini, bado inaelezwa
kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa
katika vyombo vya sheria kutokana
na wahusika kuwaficha wahalifu
mara wanapotoka hospitalini.
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa
Arusha Maria Maswa akizungumza
wakati alipotembelea waathirika wa
matukio ya unyanyasaji wa kijinsia
katika hospitali ya mount
Meru,amesema yanapotokea matukio
hayo,walengwa wamekuwa wagumu
kutoa ushirikiano kwa madai ya
kumaliza swala hilo kinyumbani
hatua inayochochea ukuaji wa
matatizo hayo.Maria Maswa-Afisa
Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi.
Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio
hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha
limeeleza kuwa linaendelea na msako
dhidi ya Mama Tatu Msuya
anayedaiwa kutekeleza kitendo
hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya
kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi
cha mwezi november 2012 mpaka
sasa.
Picha zote na habari kwa hisani ya
Gadiola Emanuel wa
.
Wazalendo 25

1 comment:

.