Friday, December 13, 2013

Kaseja aongezewa dozi maalum Yanga


KOCHA wa Makipa wa Yanga, Razack Siwa
amewaongezea program ya mazoezi makipa
wake, Juma Kaseja, Ali Mustapha ‘ Barthez ’
na Abdul Yusuph ikiwa ni siku chache tangu
Kaseja ajiunge na timu hiyo katika usajili wa
dirisha dogo .
Akizungumza na Championi Ijumaa , Siwa
alisema program hiyo aliyoitoa ya kwenda
kujifua kwenye Ufukwe wa Coco , Masaki jijini
Dar es Salaam, itakuwa ya wiki mbili, lengo
likiwa ni kuwaweka fiti makipa wake kwa ajili
ya mzunguko wa pili wa ligi .
“Katika kuhakikisha makipa wangu wanakuwa
fiti kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi ,
nimeweka program mpya ya kufanya
ufukweni .
“Ujue kipindi hiki ndiyo kizuri kwa kuwapa
wachezaji mazoezi magumu kwa kuwa ligi
imesimama , inapoanza wanafanya mazoezi
mepesi pekee, ” alisema Siwa.

No comments:

Post a Comment

.