Sunday, December 8, 2013

AS Cannes yamfuata Kapombe Tanzania


Na Khadija Mngwai
KLABU ya AS Cannes ya nchini Ufaransa,
imemfuata beki wake Shomari Kapombe kwa
kutuma nyaraka kwenye ubalozi wa Ufaransa
nchini , ili nyota huyo wa zamani wa Simba
aweze kupata visa .
Kapombe amekwama nchini kufuatia kukosa
visa ya kumrudisha Ufaransa kwa kuwa ile
aliyokuwa nayo awali , imeisha muda wake.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania
( TFF ) , Boniface Wambura , alisema Klabu ya
AS Cannes imetuma mikataba yote ya
Kapombe aliyosaini na klabu hiyo pamoja na
nyaraka mbalimbali katika ubalozi wa
Ufaransa hapa nchini kwa lengo la kumsaidia
apate visa kwa haraka .
“Klabu ya AS Cannes anayoichezea Kapombe,
tayari imeshatuma mikataba pamoja na
‘ dokumenti ’ mbalimbali katika ubalozi wa
Ufaransa hapa nchini ili kuweza kusaidia juu
ya upatikanaji wa visa ya Kapombe.
“Klabu hiyo inamhitaji mchezaji huyo kwa
haraka na jambo tunalolifanya hivi sasa ni
kuhakikisha anapata visa ya muda mrefu
itakayomuwezesha kukaa Ufaransa kwa
kipindi kirefu bila shida,” alisema Wambura

No comments:

Post a Comment

.