Sunday, December 8, 2013

Tambwe , Kaze kutua Dar kesho


Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba,
Gilbert Kaze ( katikati) na Amissi Tambwe
( kulia ) .
Na Lucy Mgina
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba,
Amissi Tambwe na beki wa timu hiyo , Gilbert
Kaze, wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es
Salaam kesho Jumanne tayari kwa kuanza
mazoezi na wenzao .
Kocha wa Simba, Mcroatia , Zdravok
Logarusic , aliwachimba mkwara kwa kudai
atawakata mishahara nyota wote ambao
walichelewa kujiunga na kikosi hicho
kilichoanza mazoezi Jumatatu ya wiki
iliyopita kwenye Uwanja wa Kinesi .
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Tambwe alisema awali walitaarifiwa warudi
nchini Alhamisi ya wiki iliyopita lakini yeye
akaomba kuwa atarejea Jumanne ya wiki hii
ambayo ni kesho .
Alisema tayari wameshaomba watumiwe
tiketi ya ndege itakayoonyesha safari itakuwa
Jumanne ya kesho .
“Sisi tutakuja huko Jumanne ( kesho ) , awali
walituambia tuje Alhamisi ya wiki iliyopita
lakini nikawaambia tutakuja Jumanne ,
tumeomba watutumie tiketi , kwa hiyo
tunasubiri na mpaka leo ( juzi ) bado
hatujapata,” alisema Tambwe.

No comments:

Post a Comment

.