Sunday, December 8, 2013

Rais Kikwete amuandikia barua Tenga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Jakaya Mrisho Kikwete.
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Jakaya Mrisho Kikwete , amemuandikia barua
Rais Mstaafu wa Shirikisho la Soka Tanzania
( TFF ) , Leodegar Tenga , akimshukuru kwa
mchango wake wa kuliendeleza soka la
Tanzania .
Katika barua yake hiyo , Rais Kikwete
amemtaka Tenga asichoke kutoa ushauri na
uzoefu wake kila utakapohitajika katika
shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo
ya mpira wa miguu Tanzania .
Rais Kikwete alikuwa akiijibu barua ya Tenga
iliyokuwa ikimuarifu kuhusu kumaliza kipindi
chao cha uongozi na kumshukuru yeye binafsi
( Rais Kikwete ) na serikali anayoiongoza kwa
mchango waliotoa katika kuendeleza mpira
wa miguu nchini .
“Pongezi zako zimetupa moyo na ari ya
kuongeza maradufu juhudi zetu za kuboresha
kiwango cha ubora wa mchezo wa mpira wa
miguu nchini .
“Kwa niaba ya serikali , napenda kuchukua
nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwako
wewe na uongozi wote uliopita wa TFF kwa
mchango wenu muhimu mlioutoa wa
kuendeleza mpira wa miguu nchini .
“Mafanikio ya kutia moyo yamepatikana
chini ya uongozi wako , ” alisema Rais Kikwete
katika barua yake hiyo na kumtakia kila la
heri Tenga katika shughuli zake .
Tenga ambaye hivi sasa ni mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka
Afrika ( Caf ) na Mwenyekiti wa Baraza la
Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
( Cecafa ) , aliiongoza TFF kwa vipindi viwili
kuanzia Desemba 2004 hadi Oktoba 2013 .

No comments:

Post a Comment

.