AMA kweli haki hakuna .
Katika hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja
Elias John , mkazi wa Kigamboni jijini Dar ,
( 28) amejikuta katika wakati mgumu wa
kupofuka baada ya kuchomwa sindano
inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia
kujihusisha kimapenzi na mwanamke
anayedaiwa kuwa ni mke wa askari Polisi.
Elias John , mkazi wa Kigamboni jijini Dar ,
( 28 ) baada ya kupofuka macho.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es
Salaam, Elias alidai alikumbwa na mkasa huo
mwaka 2011 wakati akiwa na uhusiano wa
kimapenzi na mwanamke aliyemtaja kwa jina
moja la Amina, ambaye pia alijihusisha na
polisi aliyemtaja kwa jina moja la James ,
aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha
Polisi cha Kilwa Road, jijini Dar es Salaam.
“Polisi huyo alikuwa akinifuata mara kwa
mara na kuniambia kuwa niachane na
mwanamke huyo , lakini kwangu ilikuwa
ngumu kwa sababu tulipendana sana, ”
alisema kijana huyo.
Alisema siku ya tukio , akiwa kijiweni , polisi
huyo akiambatana na wenzake , walifika na
kumkamata bila kosa lolote na kumpeleka
katika kituo kidogo cha polisi Mianzini,
Temeke .
Elias John katika pozi akiwa na fimbo yake
ya watu wasioona .
Wakiwa kituoni hapo, kijana huyo alisema
kwa pamoja Polisi hao walimshika mikono na
miguu wakati James alichukua sindano na
kumchoma .
Akiwa hajui hatima yake, Elias alisema mara
tu baada ya kuchomwa sindano hiyo , alisikia
maumivu makali yaliyopanda hadi kichwani
na ghafla akapoteza uwezo wake wa kuona .
“Siwezi kuelezea zaidi maumivu niliyoyapata
baada ya kuchomwa sindano ile na hapo
hapo macho yangu hayakuweza kuona tena
licha ya kujitahidi sana, ” alisema .
Macho ya Elias yalivyoharibiwa na sindano
inayodawa kuwa ya sumu.
Alisema baada ya kuchomwa sindano hiyo ,
askari hao walimtaka aondoke na akajitahidi
kuwapa taarifa ndugu zake , ambao
walimchukua na kumpeleka Muhimbili
ambako hata hivyo walishindwa kumsaidia na
hata alipopelekwa CCBRT , pia ilishindikana .
Katika hali ya kusikitisha zaidi , ndugu zake
walijaribu kufuatilia suala hilo polisi , lakini
walipofika waliambiwa kirahisi kwamba
askari hao wote walishafukuzwa kazi .
Alisema juhudi za ndugu zake kuhakikisha
haki inatendeka zimegonga mwamba licha ya
suala lake kufikishwa kwa taasisi za haki za
binadamu ambako bado linashughulikiwa,
ingawa hakuna matumaini ya kupatikana kwa
ufumbuzi .
“Maisha yangu yamekuwa magumu sana na
sijui hatma ya kesi yangu , nitaendelea kuishi
hivi mpaka lini ? Kwa vile kwa sasa
naombaomba tu , ” alisema .
Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kuliangalia suala lake kwa
undani ili lipatiwe ufumbuzi .
Thursday, December 12, 2013
ATEMBEA NA MKE WA POLISI .APOFULIWA MACHO..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Diih kaazi
ReplyDelete