Thursday, December 12, 2013

MAHARI YA LULU LAKI 8


Na Mwandishi Wetu
Imevuja kuwa mwanaume atakayetaka
kumuoa staa wa sinema za Kibongo,
Elizabeth Michael ‘ Lulu’ atalazimika kutoa si
chini ya shilingi laki nane ( 800 , 000) kama
mahari ili kumuoa mwigizaji huyo .
Elizabeth Michael ‘Lulu ’ .
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili ,
wanaume wengi wamekuwa wakimendea
kufunga ndoa na Lulu lakini wakashindwa
njia za kumpata.
Ilidaiwa kuwa kikwazo kikubwa
wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia
na kigezo cha dini kwa sababu Lulu hataki
kuolewa na muislam kwani hayupo tayari
kubadili dini.
Akizungumza na Amani katika mahojiano
maalum, mapema wiki hii , mama wa Lulu,
Lucresia Karugila alisema kwa upande wake
yupo tayari kupokea mahari yoyote ilimradi
mwanaye awe ameridhiana na mwanaume
husika .
“Unajua Lulu ameshakua , mambo ya
kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya
kizamani.
“Siwezi kupanga mahari, sijui laki nane au
laki ngapi . Kiasi chochote ni sawa cha msingi
mwanangu awe amekubaliana na huyo
mwanaume .
“Hajaniambia kama kuna mtu anataka kuleta
mahari, ” alisema mama Lulu .
Kwa upande wake Lulu alisema : “Kwa sasa
sina wazo la kuolewa ila naweza kuamka
kesho nikabadili uamuzi. ” Alipoulizwa kama
ni kweli atatakiwa kulipiwa mahari ya laki
nane alisita kidogo.
Kuhusu kigezo cha dini staa huyo alikiri kuwa
kati ya vitu anavyozingatia ni hicho kwani
hataki mwanaume wa kumbadilisha dini na
mahari yake itategemea na mtoaji
KWA NINI LAKI 8?
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa
wanandoa wengi waliofunga pingu za maisha
hivi karibuni ulibaini kwamba wengi walilipa
mahari ya kati ya shilingi laki sita na milioni
moja na nusu huku wastani ukiwa ni shilingi
laki nane.

1 comment:

.