Thursday, December 12, 2013

MWANAMKE AJIFUNGULIA BARABARANI


Na Mashaka Baltazar , MWANZA
MWANAMKE anayefahamika kwa jina la
mama Eric , hivi karibuni muda wa saa 11 jioni
alijikuta akijifungua mtoto wa kiume
Barabara ya Posta jijini hapa kufuatia
kushikwa na uchungu ghafla .
Akina mama waliomsaidia mama Eric
kujifungua wakiwa na mtoto aliyezaliwa .
Akiwa katika hali ya kuhangaika kusukuma
mtoto , mwanamke huyo aliishiwa nguvu huku
tayari kichwa cha mtoto kikiwa kimetokeza
nje , ndipo mama mmoja aliyekuwa akisafiri
akajitokeza kumsaidia kumzalisha .
“Nilimwona akihangaika kusukuma mtoto ,
lakini akaishiwa nguvu. Nilimwonea huruma
nikatua begi na mkoba , nikamshika mikono
akaja mama mwingine tukasaidiana
kumzalisha , ” alisema mama huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Euphrazia John ,
mkazi wa Bariadi, Simiyu.
Euphrazia alisaidiana na akina mama
wengine, Juliana Wambura na mke wa diwani
wa zamani wa Kata ya Nyamagana, Mama
Mkiwa .
Baadaye wanawake hao walimpeleka mzazi
huyo nyumbani kwao Capri Point jijini hapa .
Mama Eric akiwa kwenye gari kuelekea
nyumbani.

1 comment:

.