Thursday, December 12, 2013

BAADA YA OBAMA KUONEKANA ANASALIMIANA CASTRO...WAMAREKANI WAKASIRISHWA NA KUPINGA KITENDO HICHO...JIONEE MWENYEWE HAPA


Baadhi ya Maseneta wa majimbo mbalimbali
nchini Marekani wamekosoa kitendo cha Rais
wa nchi hiyo Barack Obama kupeana mkono na
kiongozi wa Cuba Raul Castro wakati wa
kumuaga mzee Nelson Mandela Johannesburg
South Africa.
Mmoja wao ambae ni Bi Lehtinen amesema
‘wakati kiongozi wa ulimwengu huru
anaposhikana mkono na kiongozi ambae ni
dikteta inaonekana wazi kabisa kwamba hili ni
tukio lililopangwa, Raul Castro anatumia mkono
huu huu kutia saini maamuzi ya kikatili
yanayokandamiza, kunyanyasa hata watu wasio
na hatia’
‘Hivi tunavyozungumza Viongozi wa Upinzani
Cuba wanakatwa na kuteswa kwa kupigwa bila
hatia, wanafungwa gerezani na kufanyiwa
mengine ya kikatili kupitia ruhusa ya mkono
huohuo wa alioshikana nao Rais Obama’ –
Lehtinen.
Pamoja na kushikana mkono na Raul, Rais
Obama kwenye hotuba yake aliyoitoa muda
mfupi baadae alionekana kumpa madongo Raul
kwa kuwaponda wanaomlilia Mzee Mandela
wakati wao wenyewe wanashindwa kutekeleza
yale mazuri aliyokua akiyafanya ikiwemo siasa
za kistaarabu.
Wengine waliopinga kitendo cha Rais Obama
kumsalimia Raul kwa kupeana mikono ni Seneta
John McCain ambae amesema hiki kitendo ni
sawa na kupeana mkono na Adolf Hitler na
kusisitiza ‘kwa nini upeane mkono na mtu
ambae bado anawashikilia Wamarekani kwenye
magereza yake?’

No comments:

Post a Comment

.