Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na Johnson
Nguza ‘Papii Kocha ’.
Stori:Na Mwandishi wetu
NGUZA Mbangu, mtoto mkubwa wa
mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi
anayetumikia kifungo cha maisha jela , Nguza
Viking maarufu kama Babu Seya, amesema
mzazi wake pamoja na mdogo wake , Papii , ni
lazima wataachiwa huru hivi karibuni .
Mbangu, ambaye pia hufahamika kisanii
kama Mashine, ambaye hivi sasa ni
mwinjilisti , alitoa kauli hiyo hivi karibuni
alipozungumza na gazeti hili , akisema kuwa
kutolewa jela kwa ndugu zake hao ,
kutawafanya Watanzania kumsujudia Mungu
kupitia tukio hilo.
“Amini nakuambia , Mungu amenipa maono ,
Babu Seya na Papii wako huru, watatoka tu ,
kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko
mbali, ni lazima watatoka kwa sababu
hawana hatia , ” alisema Mbangu, ambaye pia
alihukumiwa kifungo cha maisha jela kama
mzazi wake , lakini akaachiwa wakati
walipokata rufaa kwa mara ya kwanza
mahakamani.
Alisema tukio hilo litakapotokea, litawafanya
Watanzania wote kumsujudia mwenyezi
Mungu , kwa sababu litakuwa ni ishara ya
uwezo wake katika kutenda maajabu .
Babu Seya na Papii walihukumiwa kifungo
cha maisha jela mwaka 2004 baada ya
kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa
Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Sinza . Hata
hivyo , jitihada zao za kujinasua kwa mara ya
mwisho ziligonga mwamba hivi karibuni
baada ya jopo la majaji watatu kutupilia
mbali maombi ya kuachiliwa huru baada ya
kufanya mapitio ya kesi hiyo iliyovuta hisia
za watu wengi nchini .
Tuesday, December 10, 2013
BABU SEYA , PAPII LAZIMA WATAACHIWA HURU '
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jamaniiii dah
ReplyDeleteWatapata tu msamaha tuwaombee
ReplyDelete