Tuesday, December 10, 2013

BABY MADAHA ANUSIRIKA KUBAKWA


STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph
Madaha ‘Baby Madaha’ amenusurika kubakwa
na vijana wa kihuni nchini Kenya maarufu kama
machokoraa.
Tukio hilo lilitokea pande za Mombasa nchini
Kenya wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi
video ya wimbo wake uitwao The Gal Bladder
ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima
na kuanza kumkimbiza Baby Madaha.
“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa wakati
meneja wangu akinielekeza matakwa ya video
hiyo ambayo yalihitaji vijana wa mtaani, ghafla
wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka
kunibaka. Bahati nzuri nilifanikiwa kutimua mbio
na kuwazidi,” alisema Baby.

1 comment:

.