Tuesday, December 10, 2013

RONALDO, RIBERY NA MESSI KUCHUANA TUZO YA MCHEZAJI BORA


FIFA imethibitisha orodha ya majina ya
wachezaji watatu walioingia Fainali ya kuwania
tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka
2013, Ballon d'Or ambao ni mtetezi Lionel Messi,
Cristiano Ronaldo na Franck Ribery.
Messi ameshinda mfululizo mara nne tuzo
zilizopita, lakini safari hii ni Ronaldo anayepewa
nafasi kubwa ya kutwaa mpira wa dhahabu.
Mtu wa tuzo: Lionel Messi aliposhinda tuzo ya
2012 ya Ballon d'Or
Watatu wa Fainali: Mwaka jana walioingia fainali
walikuwa Cristiano Ronaldo, Andres Iniesta na
Messi
Mshindi mtarajiwa: Messi anaweza kupokonywa
tuzo hiyo na Ronaldo kutokana na mchezaji huyo
Real Madrid kuwa juu hivi sasa
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, amefunga
mabao 32 tayari msimu huu kwa klabu na timu
yake ya taifa, huku Messi kwa sasa yupo nje ya
kikosi cha Barcelona kutokana na maumivu ya
nyama.
Mabao yake matatu aliyofunga peke yake, hat-
trick wakati Ureno inaifunga 3-2 Sweden katika
mechi maalum ya kufuzu Kombe la Dunia,
yameongeza hamasa za watu kumpendekeza
kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili katika
historia yake.
Ribery, aliyeiwezesha Bayern Munich kutwaa taji
la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alikuwa anapewa
nafasi kubwa ya kuishinda kabla ya Ronaldo
kufanya mambo makubwa dhidi ya Sweden na
FIFA ikaongeza muda wa kupigia kura
washindani.
Mshindi atatangazwa katika usiku wa hafla
maalum ya Ballon d'Or mjini Zurich, Usiwis
Januari 13, mwakani.
Wakati huo huo, FIFA pia imethibitisha orodha ya
wachezaji wanaowania kuwamo katika kikosi cha
wachezaji 11 bora wa dunia, FIFPro World XI
2013.
Kuna wachezaji wanne wa England kwenye
orodha hiyo ambao ni Leighton Baines, Ashley
Cole, Steven Gerrard na Wayne Rooney.
Makipa:
Gianluigi Buffon (Italy, Juventus); Iker Casillas
(Spain, Real Madrid CF); Petr Cech (Czech
Republic, Chelsea FC); Manuel Neuer (Germany,
FC Bayern München), Víctor Valdes (Spain, FC
Barcelona).
Mabeki:
David Alaba (Austria, FC Bayern München);
Jordi Alba (Spain, FC Barcelona); Dani Alves
(Brazil, FC Barcelona); Leighton Baines
(England, Everton FC); Jérôme Boateng
(Germany, FC Bayern München);Ashley Cole
(England, Chelsea FC); Dante (Brazil, FC
Bayern München); Mats Hummels (Germany,
Borussia Dortmund); Branislav Ivanović (Serbia,
Chelsea FC); Vincent Kompany (Belgium,
Manchester City FC); Philipp Lahm (Germany,
FC Bayern München); David Luiz (Brazil,
Chelsea FC); Marcelo (Brazil, Real Madrid CF);
Pepe (Portugal, Real Madrid CF); Gerard Piqué
(Spain, FC Barcelona); Sergio Ramos(Spain,
Real Madrid CF ); Thiago Silva (Brazil, Paris
St-Germain FC); Raphaël Varane (France, Real
Madrid CF); Nemanja Vidić (Serbia, Manchester
United FC); Pablo Zabaleta (Argentina,
Manchester City FC).
Viungo:
Xabi Alonso (Spain, Real Madrid CF); Gareth
Bale (Wales, Tottenham Hotspur FC/Real
Madrid CF);Sergio Busquets (Spain, FC
Barcelona); Steven Gerrard (England, Liverpool
FC); Andrés Iniesta (Spain, FC Barcelona); Isco
(Spain, Málaga CF/ Real Madrid CF); Mesut
Özil (Germany, Real Madrid CF/Arsenal FC);
Andrea Pirlo (Italy, Juventus); Marco Reus
(Germany, Borussia Dortmund); Franck Ribéry
(France, FC Bayern München), Arjen Robben
(Netherlands, FC Bayern München); Bastian
Schweinsteiger(Germany, FC Bayern München);
Yaya Touré (Côte d’Ivoire, Manchester City FC);
Arturo Vidal (Chile, Juventus); Xavi (Spain; FC
Barcelona).
Washambuliaji:
Sergio Agüero (Argentina, Manchester City FC);
Mario Balotelli (Italy, Manchester City FC/AC
Milan); Edinson Cavani (Uruguay, SSC Napoli/
Paris Saint-Germain FC); Diego Costa (Spain,
Club Atlético de Madrid); Cristiano Ronaldo
(Portugal, Real Madrid CF); Didier Drogba (Côte
d’Ivoire, Shanghai Shenhua FC/Galatasaray
SK); Radamel Falcao (Colombia, Club Atlético
de Madrid/AS Monaco FC); Zlatan Ibrahimovi
(Sweden, Paris Saint-Germain FC); Robert
Lewandowski (Poland, Borussia Dortmund);
Mario Mandžukić (Croatia, FC Bayern
München); Lionel Messi (Argentina, FC
Barcelona); Neymar (Brazil, Santos FC/FC
Barcelona); Wayne Rooney (England,
Manchester United FC); Luis Suárez (Uruguay,
Liverpool FC); Robin van Persie (Netherlands,
Manchester United FC).

No comments:

Post a Comment

.