Msanii wa muziki wakizazi kipya nchini
Tanzania Baby Madaha katika poz
Hatua ya Baby Madaha kuwa msanii wa kwanza
mwanamke nchini Tanzania, kujitokeza
hadharani kumchambua msanii huyo mkubwa na
mwenye heshma kubwa ndani na nje ya nchi,
imevuta hisia za wadau wa muziki nchini huku
akimwagiwa sifa kemkem kwa kujitokeza na
kufuangua ufahamu wa wasichana kutokana na
imani kwamba Diamond ni mchawi anayetumia
nyota za wanawake kujipatia umaarufu.
Baby madaha ambaye anatarajia kuzindua Single
nne pamoja na muvi yake kali zilizotengenezwa
nje ya nchi, amesema kwamba kinachomkera
zaidi ni kitendo cha Diamond kudhalilisha
wasicha wenzake kimapenzi, kila kukicha kutoka
na uwezo wake wa kifedha huku akitangaza wazi
kwamba anafanya mapenzi bila kutumia kondom
kwa madai kwamba anatafuta mtoto.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania,Baby Madaha akiwa katika
poz,Akizungumza na Habarimpya.com Baby
Madaha alisema kwamba,uzinduzi wa kazi yake
itafanyika katika Hotel ya Golden Tulip ambapo
atatumia uzinduzi huo kumwonyesha Diamond
kwamba wanawake si chombo cha starehe kama
anavyo fikiria, huku akimwonyesha kwamba yeye
ni Queen Of Swagg (QOS), na kwamba staili hiyo
itafunika staili ya ngololo ya single moja
iliyobeba uchafu wa ngono na uchawi ndani ya
Album yake iliyozinduliwa katika Hotel ya Serena
jijini Dar es Salaam.
"Tarehe 22 Jumapili Disemba mwaka huu pale
Golden Tulip nitamuonyesha Diamond,kuwa
Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua
Single moja ya ngololo pale Serena mimi
ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack na
Move yangu mpya ya the Galbladder,
iliyonigarimu mamilioni kuitengeneza nje ya
nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein
ambao pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy&
candy ya jijini Nairobi, huku mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya
Rais Kikwete pale Magogoni jijini Dar es
Salaam"alisema Baby Madaha.
Kuhusu kauli yake kwamba Diamond ni mchawi
alisema kwamba, "ingawa kuna maneno mengi
kwamba Diamond ni mchawi na kwamba
anaweza kuniroga, mimi hilo halinitishi kwa
sababu yeye anashindana na wanawake badala
ya kushindana na wanaume wenzake, katika
maendeleo ila ukweli ni kwamba mimi si shindani
na wanwake kwa sababu ni marafiki zangu, ila
ninashindana na wanaume katika suala la
maendeleo na siamini katika uchawi na akiona
kwamba anaweza kuniroga kama ambavyo watu
wake wananitangazia ajaribu,kwani mimi
ninazungukwa na nguvu za Mungu na si Nguvu
na Mganga wa kienyeji".
Baby Madaha alisema kwamba baada ya
kumwangusha nyota huyo wa muziki nchini na
kumfanya afikirie kumroga katika uzinduzi huo
ataanza kufanya ziara nchini nzima kuitangaza
Queen of Swagg itakayozidi kuipoteza ngololo ya
Diamond katika ramani ya muziki ndani na nje
ya nchi, kabla ya kuendelea na show kali
sehemu mbalimbali Dunaini kama ilivyo pangwa
na wanadhamini wkake wakuu Heinekein.
Sunday, December 15, 2013
BABY MADAHA AZIDI KUMUANDAMA DIAMOND, ABAINI HILA ZA DIAMOND PLATNUMZ........ATOBOA SIRI NZITO ILIYOJIFICHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wanajuana hawa sio bure
ReplyDeleteNDO KIKI HIYO ANATANGAZA KIJANJA HIYO SHOW
ReplyDelete