Friday, December 13, 2013

Wachezaji Yanga waomba kuonana na Manji


Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini .
Na Wilbert Molandi
WACHEZAJI wa Yanga wameomba kuonana
na mwenyekiti wao , Yusuf Manji kwa ajili ya
mazungumzo kabla ya kumaliza muda wake
baada ya kusema hana mpango wa
kugombea uongozi klabuni hapo mara baada
ya muda wake wa kuwepo madarakani
kumalizika .
Yusuf Manji.
Akizungumza na Championi Ijumaa, nahodha
wa Yanga, Nadir Haroub ‘ Cannavaro’ ,
alisema hajajua sababu ya mwenyekiti huyo
kutopanga kugombea tena , hivyo kwa niaba
ya wenzake ameomba wakutane kwa ajili ya
kuzungumza naye masuala kadhaa .
Cannavaro alisema mwenyekiti bado
anahitajika katika timu hiyo katika kuleta
maendeleo na hasa kipindi hiki ambacho timu
hiyo inajiandaa kwa mzunguko wa pili wa
Ligi kuu Bara pamoja na michuano ya
kimataifa mwakani.
“Ujue hadi hivi sasa wachezaji
kinachoendelea kuhusiana na Manji kujitoa
Yanga hatukijui vizuri, kikubwa
tunachokiomba ni kukutana na mwenyekiti .
Ninaamini ni kiongozi bora atakayeipa
maendeleo na mafanikio timu yetu, ni vema
akaendelea kuiongoza Yanga, ” alisema
Cannavaro.
Straika wa timu hiyo , Jerry Tegete , naye
alisema : “Mimi sijui chochote kinachoendelea ,
kikubwa nasikia amejitoa Yanga, hivyo ni
vema tukakutana naye kwa ajili ya
kuzungumza naye ili kujua kinachoendelea

1 comment:

.