Barcelona na Real Madrid wamepigwa faini ya zaidi
ya£2.5million kila timu baada ya kuvunja sheria ya
kusaini mkataba wa muda mrefu wa haki za
matangazo ya TV.
Mikataba hiyo baina ya vilabu hivyo na kampuni ya
Mediapro imevunja sheria ya nchi hiyo kupitia
mamlaka ya ushindani wa kibiashara - inayokataza
kuwepo kwa mkataba wa zaidi ya miaka mitatu
baina ya vilabu na kampuni ya matangazo ya TV.
Comisión Nacional de la Competencia imefikia
uamuzi kwamba vilabu hivyo viwili, pamoja na
Sevilla na Racing Santander, vilivunja sheria
iliyotungwa mwaka 2010 inayozuia mikataba ya
matangazo ya TV kuzidi miaka mitatu.
Real Madrid imepigwa faini ya £3.2m na Barcelona
£2.9m wakati Mediapro watalipa faini ya £5.3m.
Sevilla imepigwa faini ya £745,000 na Racing
Santander ambao kwa sasa wapo ligi daraja la 3
wakiwa na ukata mkubwa wa uchumi watalazimika
kulipa £24,800.
Mediapro inawalipa Madrid na Barça kiasi cha
£115m kwa mwaka kwa manunuzi ya haki ya
mechi zao za nyumbani lakini vilabu vyote viwili
vimeambiwa na mamlaka za Spain kwamba ni
lazima viache kufanya dili zao binafsi za
matangazo ya TV na kujiunga na vilabu vingine
katika dili hizo kuanzia mwaka 2016.
Endapo Madrid na Barcelona watajiunga na vilabu
vingine katika dili za matangazo ya TV basi
mapato yao yatapungua.
Wednesday, December 4, 2013
BARCELONA NA MADRID WAPIGWA FAINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment