Monday, December 16, 2013

Bausi aitwa kuinoa Sudan Kusini


KOCHA Mkuu wa Zanzibar Heroes, Salum
Bausi, amepata taarifa njema baada ya
kufuatwa na viongozi wa Chama cha Soka
Sudan Kusini ( SSFA ) wakitaka huduma yake .
Akizungumza na Championi Jumatatu, Bausi
ambaye alikiongoza kikosi hicho cha Zanzibar
kilichotolewa katika hatua ya makundi ya
michuano ya Chalenji iliyofanyika jijini Nairobi
nchini Kenya wiki mbili zilizopita, alisema
alifuatwa na mwenyekiti wa chama hicho na
kufanya naye mazungumzo ya awali .
Bausi amesema mara baada ya mazungumzo
hayo ya awali , mwenyekiti huyo ambaye
hakumtaja jina, aliahidi kumtafuta siku
chache zijazo .
Sudan Kusini kwa sasa inanolewa na kocha
raia wa DR Congo , Malisi Kibaso .
“Nilizungumza na kiongozi wao ambaye ni
mwenyekiti wa chama , akaniambia nia yao
ya kunihitaji kukifundisha kikosi cha nchi yao
ya Sudan Kusini, tumezungumza
mazungumzo ya awali , ameniambia kuwa
atakapofika kwao atanitafuta mara moja ,”
alisema Bausi .
“Binafsi nipo tayari, naweza kwenda
kufundisha huko, mwenyekiti wao
ameniambia mengi kuwa wanataka
kumuondoa kocha wao wa sasa na
anakwenda kwao kuzungumza na viongozi
wenzake na baada ya hapo atanitafuta .”

No comments:

Post a Comment

.