BEKI mpya wa Ashanti United , Victor Costa ,
amesema atafanya jitihada zake zote katika
timu hiyo kuhakikisha inafanya vizuri kwenye
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Beki huyo wa zamani wa Simba, alisajiliwa
klabuni hapo wiki iliyopita pamoja na akina
Mohammed Banka aliyekuwa akikipiga
Bandari FC ya Kenya, Juma Jabu , Mnigeria
Ikebright Obina ( African Lyon) , Kilungo
Kassim ( Azam B ) na kipa Juma Mpongo
( Coastal Union) .
Akizungumza na Championai Jumatatu,
Costa alisema kwa sasa Ashanti ina kila
sababu ya kufanya vizuri kwenye ligi
kutokana na usajili walioufanya kwenye
dirisha dogo lililofungwa jana usiku , hivyo
kazi imebaki kwao kuhakikisha timu hiyo
inarudi kwenye hadhi yake .
Alisema uwepo wa wakongwe kama Banka ,
Jabu kwenye timu hiyo , wakishirikiana vyema
na wachezaji wengine waliowakuta hapo ,
utaipa mafanikio timu hiyo inayoshika nafasi
ya 12 , ikiwa na pointi 10 kwenye msimamo
wa ligi .
“Unajua mara ya kwanza wachezaji wengi
walikuwa ni wageni ligi kuu, sasa hivi
wameshazoea , halafu pia ujio wa Banka ,
Jabu, mimi na wengine utaipeleka Ashanti
mbali zaidi , pengine tunaweza kumaliza hata
kwenye nafasi ya pili au ya tatu , ” alisema
Costa.
Monday, December 16, 2013
Costa aapa kuipaisha Ashanti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment