Monday, December 16, 2013

Kizuguto: Mimi siyo msemaji Yanga SC


MSEMAJI wa Yanga, Baraka Kizuguto,
amedai yeye siyo msemaji wa klabu hiyo na
kutaka waandishi kutomfuata .
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Kizuguto alisema kuwa yeye siyo msemaji wa
klabu hiyo kama watu wanavyodhania,
badala yake mtu yeyote anaweza kuwa
msemaji wa Yanga.
“Nashangaa watu wanavyonifuata na kusema
mimi ni msemaji, mimi siyo msemaji wa
Yanga, mimi ni ofisa habari tu , kwani mtu
yeyote anaweza kuzungumza habari za klabu
na si mimi .
“Kuna watu wengi ambao wanaweza
kuzungumza, kama ulikuwa haujui ni wewe tu
lakini kila mmoja anajua , ” alisema Kizuguto
ambaye amekuwa na mbwembwe nyingi
zisizo za msingi kila anapoulizwa masuala
mbalimbali ya klabu yake hiyo .

No comments:

Post a Comment

.