Na Nicodemus Jonas
BEKI wa zamani wa Simba, Amri Said
anaamini Simba ya sasa haiwezi kupata
mafanikio iwe ni katika ligi ya ndani au nje
ya Tanzania katika kipindi cha miezi sita
ambayo Zdravok Lugarusic amepewa .
Said amewahi pia kuwa kocha msaidizi wa
timu hiyo , japokuwa kwa sasa anaifundisha
Ndanda FC. Amesema suala la mafanikio
litakuwa gumu kwani kila kocha huwa na
falsafa yake na huhitaji muda ili kuzoea
wachezaji.
“Simba isitarajie kupata mafanikio kwa miezi
hii sita aliyopewa kocha . Kwanza, kila kocha
huwa na falsafa yake ambapo huhitaji muda
wa kutosha ili wachezaji waizoee kabla ya
kuanza kutafuta mafanikio .
“Haiwezekani ndani ya miezi hii awe amepata
first eleven ( kikosi cha kwanza) , hapohapo
aanze kukimbiza ubingwa, ” alisema Said .
Lugarusic amesaini mkataba wa miezi sita
kuitumikia timu hiyo ambayo katika raundi ya
kwanza ilikuwa chini ya Kocha Abdallah
Kibadeni.
Friday, December 13, 2013
Beki Simba : Mzungu hawezi kuipa Simba ubingwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment