Friday, December 13, 2013

Mama amzuia Mganda kurudi Coastal


Na Martha Mboma
MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Lutimba
Yayo, raia wa Uganda , ameshindwa kuwasili
nchini akitokea Uganda kwa wakati kutokana
na kumuuguza mama yake mzazi .
Yayo ameanza kuichezea Coastal msimu huu
akitokea URA ya Uganda na aliweza kuwika
nchini baada ya kuzifunga timu za Simba na
Yanga katika mechi za kirafiki .
Akizungumza na Championi Ijumaa kutokea
Uganda, Yayo alisema : “Nilitakiwa kurejea
mapema ili kuweza kuungana na wenzangu
kwa ajili ya kuanza maandalizi lakini
imeshindikana.”

No comments:

Post a Comment

.