Monday, December 16, 2013

Beki Yanga atua Villa Squad


HATIMAYE beki wa zamani wa Yanga,
Godfrey Taita , amemwaga wino kuitumikia
Villa Squad inayoshiriki Ligi Daraja la
Kwanza Tanzania Bara .
Beki huyo aliyeachwa na Yanga msimu
uliopita baada ya kumaliza mkataba wake,
ataanza kuonekana na uzi wa Villa yenye
maskani yake Magomeni , kwenye mzunguko
wa pili wa ligi hiyo unaotarajiwa kuanza
Februari, mwakani.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Katibu
Mkuu wa Villa , Aboubakar Kasanda , alisema
wamemsajili mchezaji huyo kutokana na
umahiri wake anapokuwa uwanjani ili
aiimarishe safu ya ulinzi ya timu hiyo .
“Tulihitaji beki wa kuja kukiongezea nguvu
kikosi chetu kwenye mzunguko wa pili ,
tukaona Taita atatufaa zaidi kutokana na
uwezo wake ambao hadi leo bado anao
tangu alipoondoka Yanga, tunaamini
atatusaidia sana kwenye mzunguko wa pili , ”
alisema Kasanda .
Villa pia imeiongezea nguvu safu yake ya
ushambuliaji kwa kumsajili kiungo
mshambuliaji wa Coastal Union ya Tanga,
Lameck Mbonde .

No comments:

Post a Comment

.