Kocha Mkuu wa Simba , Zdravko Logarusic.
Na Mwandishi wetu
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ,
amekishuhudia kikosi cha Yanga kwa dakika
90 wakati kikitoka na ushindi wa mabao 3 -2
dhidi ya KMKM lakini akaibuka na hoja mbili
muhimu huku moja kati ya hizo akisema
kocha wa kikosi hicho amemdanganya.
Akizungumza na Championi Jumatatu,
Logarusic , maarufu kwa jina la Loga ,
amesema ameiangalia Yanga ikicheza
mchezo huo juzi Uwanja wa Taifa , Dar , lakini
aligundua kuwa nyota wa timu hiyo
walicheza kawaida , akadai hilo pengine
lilitokana na maelekezo ya kocha wao , Ernie
Brandts ili kumdanganya mpinzani wake huyo
( Loga) .
Loga amesema mchezo huo bado
haukumwezesha kuweza kukisoma kikosi
hicho vizuri, ingawa jambo lingine alilolibaini
ni kwamba Yanga ina mipango mingi ya
kutengeneza nafasi za kufunga , jambo
ambalo ni lazima alifanyie kazi kwa haraka
katika timu yake.
“Nimewaona leo Yanga, lakini ni kama
wamenidanganya, ukiangalia walivyokuwa
wakicheza jana ( juzi ) , ni kama walikuwa
wameambiwa wasicheze kwa juhudi sana ,”
alisema Loga .
Monday, December 16, 2013
Logarusic aichambua Yanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment